Mabingwa
wa Ulaya Real Madrid, wataingia dimbani kucheza na Mabingwa wa Concacaf
Cruz Azul ya Mexico. Katika mchezo wa kombe la klabu bigwa ya dunia usiku wa jumanne huko mjini Marrakech nchini Morocco.
Nusu Fainali
nyingine itachezwa jumatano usiku kati ya San Lorenzo ya Argentina na
Auckland City ya New Zealand. Wakati Real wanaanza hatua ya nusu fainali, Cruz Azul walianzia robo fainali na kuibwaga Western Sydney
Wanderers ya Australia kwa Bao 3-1 katika mechi iliyopigwa dakika 120
baada ya kwenda sare ya goli 1-1 katika dakika 90 za mchezo. Real
watakuwa wakisaka taji lao la 4 kwa mwaka 2014 kitu ambacho hawajahi
kufanya baada ya kuwahi kutwaa mataji matatu ndani ya mwaka mmoja.
Real
Madrid watawakosa mastaa wao James Rodriguez na Luka Modric ambao ni
majeruhi huku Sami Khedira pekee akiwa na uwezekano wa kucheza Fainali
ikiwa watafuzu kuitoa Cruz Azul.
CHANZO: BBC SWAHILI

No comments:
Post a Comment