Pages

Thursday, December 11, 2014

CAG KUONGOZA BODI YA UMOJA WA MATAIFA

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Profesa Mussa Assad ameteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) nafasi atakayoanza kuitumikia kuanzia Januari Mosi, mwakani.
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari ilieleze kuwa, Profesa Assad kwa sasa yupo nchini Uingereza kuhudhuria mkutano wa vikao vya bodi hiyo ambayo wajumbe wake ni wadhibiti na wakaguzi wakuu wa hesabu za Serikali kutoka Uingereza, Tanzania na India.
Profesa Assad alisema ameridhishwa na mwenendo wa vikao vya UNBoA na kuahidi kushirikiana kwa karibu kufanya kazi na wajumbe wenzake wanaounda bodi hiyo.
“Nimeridhishwa na mwenendo wa bodi nawaahidi kufanya nao kazi kwa karibu na wajumbe wenzangu wote,” alisema Profesa Assad.
Nafasi ya uenyekiti wa UNBoA ilikuwa inashikiliwa na CAG Amyas Morse wa Uingereza ambaye kwa pamoja na CAG Shashi Sharma wa India wameahidi kumpa ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu waliyomkabidhiwa.

CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment