Makampuni ya ulinzi nchini Marekani na Ulaya ya magharibi yamekamata
mstari wa mbele katika biashara ya silaha mwaka 2013 kwa mujibu wa
ripoti ya taasisi ya uchunguzi wa masuala ya amani ulimwenguni-SIPRI
Biashara ya vifaa vya kijeshi na huduma iliyofanywa na makampuni 100
makubwa ya silaha imefikia jumla ya dala bilioni 402,ikipungua kwa asili
mia mbili ikilinganishwa na mwaka 2012-taasisi ya SIPRI imesema katika
ripoti yake. Miongoni mwa makampuni 100 makubwa yaliyoorodheshwa,38 yana makao yake
nchini Marekani,moja nchini Canada na 30 katika nchi za Ulaya ya
Magharibi.Kwa pamoja makampuni hayo yanafikia asili mia 85 ya biashara
jumla ya silaha kwa mwaka 2013.
Biashara kutoka makampuni 10 ya silaha ya Urusi yaliyoorodheshwa na
SIPRI, inafikia jumla ya dala bilioni 31,ikiongezeka kwa asili mia 20
ikilinganishwa na mwaka 2012.Kampuni kubwa zaidi la silaha la Urusi
Almaz Antei linakamata nafasi ya 12 ikilinganishwa na nafasi ya 14 mwaka
2012.
Urusi imepania kujiimarisha kijeshi
Pato jumla limepungua mwaka 2013-kwa mara ya tatu mfululizo,na
kusalia kuwa chini kuliko la mwaka mmoja kabla kutokana na kuongezeka
biashara ya silaha kutoka Urusi na kuongezeka mahitaji kutoka
Brazil,India,Korea ya kusini na Uturuki miongoni mwa nchi nyenginezo.
Makampuni ya China hayahusiki na hesabu hizo kuitokana na ukosefu wa
maelezo kuhusu biashara ya silaha ya nchi hiyo.Taasisi hiyo ya mjini
Stockholm inayaochunguza masuala ya amani ulimwenguni imesema katika
ripoti yake huenda makampuni tisaa ya China yakakutikana miongoni mwa
mia moja yanayouza silaha.
Kuongezeka biashara ya silaha nchini Urusi kunatokana na kuongezeka
biashara ya nje pamoja na kuimaarishwa mnamo miaka ya hivi karibuni
makampuni kadhaa ya silaha yanayomilikiwa au yanayosimamiwa na
serikali-mtaalam wa taasisi ya SIPRI,Siemon Wezeman amesema katika
mahojiano na shirika la habari la Ujerumani dpa. "La muhimu kabisa ni kwamba bajeti ya kijeshi ya Urusi inaongezeka"
amesema na kuongeza tunanukuu:"Urusi imepania kuvigeuza vikosi vyake
viwe vya kimambo leo."Mwisho wa kumnukuu. Miongoni mwa changamoto zinazoikabili sekta ya silaha nchini Urusi ni
pamoja na kurekebisha vifaa na nguvu kazi na pia suala kama Urusi
itamudu kuendelea na mipango mikubwa mikubwa na ghali ya ulinzi,kuanzia
nyambizi,kupitia ndege za kivita hadi kufikia silaha ndogo ndogo.
Ushirikiano pamoja na nchi nyengine,ikiwa ni pamoja na China na India ni mojawapo ya mikakati.
Lockheed Martin na Boeing ya Marekani yanaongoza
Kuondoshwa vikosi vya Marekani nchini Afghanistan na Irak ni
mojawapo ya sababu za kupungua kwa asili mia 4.5 biashara ya silaha ya
Marekani.Hata hivyo makampuni 6 ya Marekani yameorodheshwa miongoni mwa
makampuni kumi makubwa ikiwa ni pamoja na lile Lockheed Martin
linaoongoza orodha hiyo na kufuatiwa na Boeing.
CHANZO: DW KISWAHILI
No comments:
Post a Comment