Pages

Tuesday, November 18, 2014

WAZIRI: WARIOBA ANAPEWA ULINZI

Siku chache baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, kufanyiwa vurugu wakati wa mdahalo wa Katiba iliyopendekezwa, suala hilo liliibuka bungeni jana.

Liliibuka baada ya Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema), kudai kuwa hatua ya Serikali kushindwa kuwathamini wazee inakwenda kinyume cha haki za binadamu, na kuwa hali hiyo inatokana na kukosa ulinzi.
Waziri wa Nchi, Ofisi wa Rais (Utumishi wa Umma), Celina Kombani, alisimama na kusema kuwa hivi sasa Serikali ina viongozi 13 waliostaafu ambao wanatunzwa na ofisi yake na wote wamekuwa wakipewa stahiki zao zote ukiwamo ulinzi.
Hata hivyo, alisema ofisi yake haijapata malalamiko ya Jaji Warioba kama Waziri Mkuu Mstaafu kuhusu kukosa ulinzi au kupigwa tofauti na inavyodaiwa na baadhi ya wabunge.
“Mimi ndiye Waziri na ofisi yangu ndiyo inahusika kutoa ulinzi kwa viongozi wastaafu akiwamo Warioba na kama mnaona hilo halifanyiki nendeni mkamuulize mwenyewe kama hana ulinzi wowote,” alisema na kuongeza:
“Viongozi wote tumekuwa tukiwapa ulinzi akiwemo Mheshimiwa Edward Lowassa kama Waziri Mkuu Mstaafu pamoja na Jaji Warioba…kwa hiyo wazee wanaolelewa na serikali hawajadhalilishwa na wanalelewa kama kawaida.”
Hata hivyo, kauli ya Kombani ilipingwa na Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), ambaye alisema hivi karibuni kila mtu anaelewa kwamba Jaji Warioba walivamiwa na kupigwa kwenye ukumbi wa Blue Pearl.
“Sasa Waziri unaposimama na kulieleza Bunge kwamba wazee hawa wanajaliwa vizuri, mambo ya usalama yapo sawasawa ni kutowatendea haki,” alisema na kuongeza:
“Mheshimiwa Naibu Spika, Mawaziri ambao wanatoa majibu ya namna hii tutawafanya nini wakati wanazungumza uongo…vinginevyo Mheshimiwa Kombani aombe radhi ndani ya Bunge hili?” alihoji.
Akijibu swali hilo, Kombani alisema: “Mimi ni waziri ninaowatunza wazee wastaafu, na ninachokisema nina uhakika nacho…mzee Warioba anapata huduma zote labda kama ameacha walinzi wake…analelewa na anatunzwa
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment