Pages

Thursday, October 23, 2014

UFARANSA YAKANUSHA UCHUMI WAKE KUYUMBA

Rais wa Baraza la Wawekezaji wa Kifaransa barani Afrika, Etienne GIROS akizungumza na waandishi wa habari wa Tanzania walipotembelea ofisini kwake jijini Paris, Ufaransa. Kushoto ni mtaalamu wa baraza hilo kwa ukanda wa kusini mwa Afrika, Laurent Padoux.


Ufaransa imekanusha taarifa za kuyumba kwa uchumi wao na kusisitiza kuwa bado uko imara katika maendeleo.
Akizungumza na waandishi wa habari kutoka Tanzania waliotembelea Paris, mkurugenzi wa Idara ya Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje, Gael Veyssiere alisema taarifa hizo ni propaganda za kiushindani.
Alisema ufaransa haiendeshwi kwa kuangalia takwimu za dunia na tafiti za nje kwani, licha ya takwimu zilizotolewa hakuna lililobadilika ndani ya nchi na hata kwa wananchi wake.
Veyssiere, ambaye idara yake iliratibu ziara hiyo, alisema wataendelea kuyasaidia mataifa mengine katika shughuli za kijamii na uchumi kwa ajili ya kuifanya dunia kuwa sehemu bora na salama ya kuishi binadamu wote.
Alisema Ufaransa imewekeza vya kutosha kuhakikisha uchumi wake hauathiri maisha ya wananchi na kusisitiza kuwa propaganda za washindani wao, zina nia ya kuwavunja moyo.
Alisema Ufaransa imeendelea kuzalisha na kuuza nje bidhaa zake kwa kiwango cha kuridhisha, na endapo kutatokea tatizo la uchumi, inaweza kujikwamua bila kuathiri wengine.
Uchumi wa Ufaransa unategemea zaidi viwanda, ikiwa inatengeneza ndege, magari, treni za kasi, pamoja na uuzaji wa nishati kwa baadhi ya nchi za Ulaya.
Utalii wake huchangia kiasi kidogo licha ya kuwapo kwa idadi kubwa ya watalii ambao hutembelea jiji la Paris.
Ufaransa ni ya tano kwa utajiri duniani na ya pili kwa nchi za Ulaya ikiongozwa na Ujerumani.

No comments:

Post a Comment