Pages

Tuesday, October 21, 2014

MRADI WA MAJI KUNUFAISHA WAKAZI, SHULE DAR

Shule  ya  Sekondari  Manzese, jijini Dar es Salaam na maeneo jirani na shule hiyo wanategemea kunufaika na mradi wa maji safi na usafi wa mazingira pamoja na uzalishaji wa umeme wa gesi asilia itokanayo na kinyesi cha wanafunzi wa shule hiyo.

Miradi  hiyo inatekelezwa na Mamlaka  ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kwa msaada wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN-HABITAT) huku mradi wa uzalishaji wa umeme wa gesi asilia  ya kinyesi cha binadamu ukiendeshwa na Taasisi ya Kuendeleza Nishati Asilia na Uhifadhi wa Mazingira Tanzania  (Tatedo) katika shule hiyo.
Meneja mipango wa UN-HABITAT nchini,  Phillemon Mutashubirwa, alisema miradi hiyo ilienda sambamba na uchimbaji wa visima, ujenzi wa minara ya kuwekea matenki ya kuhifadhi maji.
Mratibu wa Tatedo, Shima Sago, alisema wamegundua kuwa ni nishati ya gharama rahisi ambayo ni ya kinyesi cha binadamu kutoka kwa wanafunzi itakayokuwa na uwezo wa kuzalisha  megawati 200 za umeme na kuwa msaada kwa shule hiyo.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment