
Hata hivyo, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeichakachua sera
hiyo ya Chadema iliyowekwa katika Ilani yake ya uchaguzi wa mwaka 2010
na kusema elimu ya bure inawezekana, ingawa hadi leo chama tawala
kimeshindwa kutekeleza ahadi hiyo.
Alitoa kauli hiyo alipokuwa akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Iringa.
Alisema ajenda ya pili ya Chadema katika uchaguzi mkuu uliopita
ambayo pia wataitekeleza ni vifaa vya ujenzi kushushwa bei ili kila
Mtanzania awe na uwezo wa kujenga nyumba ya saruji na bati.
Alisema kuwa wazee wote, wafugaji, wakulima, mama lishe na makundi
mengine watapewa pensheni kwa sababu wote wamechangia uchumi wa nchi na
kwamba haiwezekani kuona wazee wanakufa hivihivi wakati wamechangia.
Ajenda ya nne alisema ni huduma bora za maji na afya ambazo ni
jukumu la serikali na siyo la mtu mmoja mmoja, lakini serikali ya CCM
imewatupia wananchi badala ya kuhakikisha wanapata huduma hiyo.
Hata hivyo, alimkosoa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana,
kwamba anazunguka nchi nzima na kuwadanganya vijana kuwa atawapatia
ajira, lakini hazungumzii kuimarisha na kujengwa viwanda.
“Kinana alisema kuwa atawapa vijana bodaboda, lakini Chadema
kinasema msigawe bodaboda, tengenezeni viwanda hapa nchini ili vijana
wapate ajira na ziuzwe kwa bei ya chini, lakini siyo wagawe bodaboda
ambazo zitawafanya wawe vilema na kusababisha nguvu kazi ya nchi
kushuka,” alisema.
Kuhusu katiba inayopendekezwa, Dk. Slaa alisema vyama vinavyounda
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vitazunguka nchi nzima mtaa kwa mtaa
na kijiji kwa kijiji katiba hiyo itakapopelekwa kwa wananchi kwa ajili
ya kupigiwa kura na kuwataka wananchi waikatae.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari, alisema
maendeleo ya Tanzania yamedumazwa na serikali kuingia katika mikataba
mibovu ambayo haijali maslahi ya wananchi na kwamba umaskini wa wananchi
umetokana na CCM huku akitolea mfano kwa sekta ya madini kuingiza
mapato madogo.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment