Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.
Serikali imekanusha kuuza eneo la Polisi
Oysterbay, jijini Dar es Salaam, bali imeingia ubia na mwekezaji
binafsi ikiwa ni miongoni mwa mikakati ya kupunguza tatizo la nyumba kwa
askari.Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira
Ame Silima, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa
Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Mosses Machali, bungeni jana.
Machali alitaka kujua kauli ya serikali kuhusiana na eneo hilo
ambalo linadaiwa kuuzwa kupitia Mpango wa Ushirikiano wa Serikali na
Sekta binafsi (PPP), ili yajengwe maduka makubwa. “Serikali ina kauli gani kuhusiana na jambo hilo wakati inasema
kuwa ina mpango wa kujenga nyumba kwa polisi,” alihoji mbunge huyo.
Silama alisema mbia huyo atajenga nyumba za polisi 350 nchini na ameanza kufanya hivyo. Naye Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini, alisema katika
wilaya ya Rombo nyumba za polisi zimejengwa kwa mabanzi na zina wadudu
aina ya kunguni na sungusungu.
Aidha, alitaka kujua kwanini serikali isihamasishe wananchi kushiriki ujenzi wa vituo vya polisi. Akijibu, Silima alimpiga kijembe Selasini kuwa ameuliza swali hilo
kwa sababu amechangia Sh. milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya
polisi.
“Mheshimiwa Selasini anataka aonekane tu, lakini amechangia Sh.
milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya polisi….Usaidie kutoa majibu
yako kwa wenzako ili Tanzania iwe na nyumba za polisi,” alisema.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment