Rais Barrack Obama wa Marekani akiwa na mtoto wake Malia.
Mwanasheria kijana nchini ametuma ombi la kumuoa mtoto wa Rais Barack Obama anayeitwa Malia.
Mwanasheria Felix Kiprono alisema jana kwamba yupo
tayari kutoa ng’ombe 50, kondoo 70 na mbuzi 30 ikiwa ni mahari ya
kumposa mtoto huyo.
Alisema kuwa analazimika kufanya hivyo ili kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kumuoa mtoto wa Rais Obama. “Nimevutiwa kumchumbia Malia tangu mwaka 2008,” alisema Kiprono baada ya kuhojiwa na gazeti la The Nairobian.
Wakati mwanasheria huyo akivutiwa na binti huyo
mwaka 2008, Obama alikuwa Rais wa Marekani katika awamu ya kwanza na
Malia alikuwa na umri wa miaka 10. “Ukweli ni kwamba sijawahi kuwa na uhusiano na
mwanamke yeyote tangu nilipovutiwa na Malia. Nimeieleza familia yangu na
wameniunga mkono,” alisema Kiprono.
Kiprono alisema ana nia ya dhati ya kumuoa Malia,
pia, ana imani kwamba wakati Obama atakapoitembelea nchi hiyo Julai,
mwaka huu atampelekea binti hiyo. “Hivi sasa nimeanza kuandika barua kwa Obama ya
kumwomba aje na Malia katika ziara yake. Nina imani kwamba ubalozi wa
Marekani nchini hapa utafikisha barua yangu kwake,” alisema Kiprono.
Mwanasheria huyo alifafanua kwamba ana nia ya
dhati ya kumposa binti huyo na wala hafuati fedha za kiongozi huyo
mweusi wa Marekani. “Watu wanaweza kufikiri kwamba nataka kuoa kwa
sababu ya fedha za familia ya Rais Obama, hiyo siyo kweli, nina mapenzi
ya dhati kwa Malia,” alisisitiza.
Mwanasheria huyo kijana ambaye hakupenda kutaja
umri wake, alisema endapo wazazi wa Malia watakubali, sherehe ya harusi
itakuwa ya kimila na itafanyika kijijini kwa wazazi wake.
Kiprono alisema baada ya kumwoa wataishi maisha ya kawaida na hawataishi maisha ya anasa. “Nitamfundisha Malia kukamua maziwa, kupika ugali na kupika chakula cha asili ya Wakalenjini kama wafanyavyo kina mama,” alisema Kiprono.
Kiprono alisema baada ya kumwoa wataishi maisha ya kawaida na hawataishi maisha ya anasa. “Nitamfundisha Malia kukamua maziwa, kupika ugali na kupika chakula cha asili ya Wakalenjini kama wafanyavyo kina mama,” alisema Kiprono.
Baba yake Obama ni Mkenya na bibi yake aliishi katika Kijiji cha Kogelo, magharibi mwa nchi hiyo.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment