Hatma
ya mvulana mwenye asili ya China anayeishi na virusi vya ugonjwa wa
ukimwi ,imetaarifiwa amelazimika kuhama nyumbani kwao baada ya
wanakijiji wapatao 200.
Kisa chake kinatanabahisha kiwango cha
unyanyapaa kwa wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini China,pindi
wanapotambulika basi hukumbana na unyanyapaa. Mlezi wa motto huyo
ambaye ni babu yake,alikuwa ni miongoni wanakijiji waishio kusini
magharibi katika jimbo la Sichuan waliosaini makubaliano ya kumuwinga
mvulana huyo mwenye umri wa miaka nane ili kulinda afya ya wanavijiji
hao .
Taarifa zinaeleza kwamba mvulana huyo aliupata ugonjwa huo
kutoka kwa mama yake mzazi,na aligunduliwa kwa mara ya kwanza kama ana
ugonjwa huo mnamo mwaka 2011, alipokwenda kupata matibabu hospitalini
baada ya kuumia.
Unyanyapaa haukuishia hapo kwa mvulana huyo kwani
kila shule aliyokwenda kutaka kujiunga nayo ilia pate elimu walimkataa,
na wanakijiji hawataki hata kuchangamana naye. Na Kunkun kwa jina
alilopewa la utani analalama akisema,hawataki hata kucheza nami,nacheza
peke yangu, na wananiona kama bomu linalotaka kulipuka wakati wowote. Pamoja
na kumnyanyapaa na kutotaka kuchangamana naye, wanakijiji hao wanadai
wanamuonea huruma,hana hatia na ni motto mdogo, lakini wakadai kuwa
virusi alivyonavyo vinawatisha.
Wanakijiji hao wanadai mama wa
mvulana huyo alifariki mnamo mwaka 2006,wakati baba wa mvulana huyo
hajulikani alipo baada ya kujua afya ya mwanawe na hivyo kumtelekeza. Elimu kwa jamii ya raia wa China juu ya ugonjwa wa ukimwi ni finyu,na hivyo kusababisha unyanyapaa na hofu miongoni mwao. Wizara
ya afya ya China na masuala ya uzazi wa mpango imeeleza takwimu
zinazoishia mwezi October mwaka huu zinaonesha kwamba watu walioathiriwa
na virusi vya ugonjwa huo ni laki nne na elfu tisini na saba,nah ii ni
tangu mgonjwa wa kwanza kugunduliwa nchini humo mwaka 1985,na
inakadiriwa kuwa china ina watu bilioni 1.36.
Suala la unyanyapaa
dhidi ya ugonjwa huo ni changamoto inayokabili shule,hospitali,maeneo ya
kazi na kwingineko nchini China,nah ii ndio sababu ya kudumaza harakati
za kutambua na kupamba na virusi hivyo.
CHANZO: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment