Wakurugenzi 17 wa halmashauri nchini,
wameshughulikiwa baada ya kuvurunda katika uchaguzi wa serikali za mitaa
uliofanyika Jumapili iliyopita.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, jana alitangaza kutengua uteuzi wa
wakurugenzi sita, kusimamisha watano, kuwapa onyo kali watatu na kuwapa
onyo wakurugenzi watatu.
Hata hivyo, licha ya makundi kadhaa ya jamii kumtaka Ghasia awajibike sambamba na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutokana na uchaguzi huo kukumbwa na kasoro nyingi, alikataa kujiuzulu. Badala yake, alisema hatawajibika kwa kuwa ameshachukua hatua dhidi ya wakurugenzi hao na kwamba amejipima na kuona anatosha.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam jana kutangaza maamuzi hayo, Ghasia alisema wakurugenzi hao wamechukuliwa hatua mbalimbali na tayari Rais ameridhia hatua hizo. "Kutokana na ripoti tulizopokea kuhusu masuala yaliyojitokeza katika uchaguzi huu, ni dhahiri kuwa wakurugenzi wa halmashauri zenye dosari wameonyesha udhaifu mkubwa katika kutekeleza jukumu la usimamizi wa uchaguzi ambalo ni moja ya majukumu ya Ukurugenzi, " alisema.
Alisema wakurugenzi hao wamefanya makosa matano ambayo ni kuchelewa kuandaa vifaa vya kupigia kura, kukosa umakini, kuchelewesha vifaa, uzembe na kutoa taarifa za kupotosha. “Kutokana na udhaifu waliouonyesha wakurugenzi hao kwa mamlaka aliyonayo chini ya Ibara ya 36 (1) (4) ya Katiba Rais ameridhia wachukuliwe hatua zifuatazo ambazo ni kutengua uteuzi, kusimamishwa kazi, kupewa onyo kali na kupewa onyo,” alisema.
WALIOSIMAMISHWA
Waziri Ghasia aliwataja wakurugenzi waliosimamishwa kazi na halmashauri zao kwenye mabano kuwa ni Felix Mabula (Hanang'), Fortunatus Fwema (Mbulu), Isabela Chilumba (Kwimba) na William Shimwela (Manispaa ya Sumbawanga). Alisema waliosimamishwa kazi ya ukurugenzi, watapisha uchunguzi zaidi wa kiwango cha ushiriki wao katika kasoro zilizojitokeza kwenye halmashauri zao.
WALIOTENGULIWA UTEUZI
Alisema wakurugenzi ambao uteuzi wao umetenguliwa ni Benjamin Majoya (Mkuranga), Abdallah Ngodu (Kaliua), Masalu Mayaya (Kasulu), Goody Pamba (Serengeti), Julius Madiga (Sengerema) na Simon Mayeye (Bunda). Alisema waliotenguliwa uteuzi watapangiwa kazi za taaluma zao wakati uchunguzi zaidi ukiendelea ili kubaini dhamira ya vitendo vyao.
WALIOPEWA ONYO KALI
Katika mtikisiko huo, wakurugenzi watatu wamepewa onyo kali ambao ni Mohamed Maje (Rombo), Hamis Yuna (Busega) na Jovin Jungu (Muheza). Kwa mujibu wa Ghasia, waliopewa onyo kali, pia watawekwa chini ya uangalizi kubaini kama wana udhaifu mwingine ili wachukuliwe hatua zaidi.
WALIOPEWA ONYO
Aidha, wakurugenzi wengine watatu wamepewa onyo ambao ni Isaya Mngulumi (Ilala), Melchizedeck Humbe (Hai) na Wallace Karia (Mvomero). Waliopewa onyo alisema wanatakiwa kuongeza umakini wanapotekeleza majukumu yao.Waziri Ghasia alisema: “Nimechukua hatua na Rais ameridhia. Mimi binafsi nimejipima naona bado natosha labda mamlaka iliyo juu yangu iamue vinginevyo.”

CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment