Polisi
mjini Manila wamevamia gereza moja na kuushangaza umma wa Philippines
baada ya kung'amua maisha ya anasa yanayoendelea ndani ya gereza hilo
kwa kikundi cha baadhi ywa wafungwa wenye upendeleo wa kipekee.
Uvamizi
huo umefanywa katika gereza hilo la Bilibid lenye wafungwa wengi nchini
humo kufuatia taarifa kwamba mtandao wa dawa za kulevya nchini humo
unafanya kazi katika gereza hilo kwa njia za panya.
Baada ya
uvamizi huo maafisa wa polisi walikuta wafungwa hao wakiwa wamefunga
viyoyozi,mabafu ya kuogea ya kisasa yenye marumaru na kupambwa kwa mawe
ya thamani,makasha ya kuhifadhia fedha,saa za gharama na fedha lukuki.
Wafungwa
hao walifanikiwa pia kununua pombe kali za gharama kubwa ,komputa na
hata simu za kisasa za gharama kubwa.kufuatia tukio hilo serikali ya
Philippine imeahidi kufanya uchunguzi wa kina.
CHANZO: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment