Sigara ya kielektroniki iliyo na bangi ndani yake imeanza kuuzwa nchini Uingereza.
Wakati sigara ya kwanza ya bangi ya kieletcroniki ilipozinduliwa mnamo mwezi juni ilikuwa ikipatikana ughaibuni pekee.
lakini sasa ,kampuni moja imechukua hatua zaidi na kuanza kuuza bidhaa hiyo katika maeneo ya Uingereza.
KanaVape
kama kinavyojulikana ni kifaa ambacho kina fanana na sigara za
kielektroniki lakini chenye Bangi, kitauzwa mitandaoni kuanzia alhamisi
ijayo,kulingana na mtandao wa Metro nchini Uingereza.
Watengezaji
wa bidhaa hiyo nchini Uingereza Atonin Cohen na Sebastien Beguerie
wanadai kwamba bidhaa hiyo ni halali kwa kuwa haina kemikali za bangi
zinazoathiri akili.
Bidhaa hiyo inatumia asilimia tano ya
bangi,ikimaanisha kuwa inampa mteja hisia za utulivu kama bangi lakini
haina athari zozote mbaya.
Bidhaa hiyo ya E-joint inamaanisha kuwa mtumiaji anaweza kuvuta mvuke wa bangi bila kupata harufu ya kawaida ya moshi wake.
Mashirika
ya madawa hatahivyo yameipinga bidhaa hiyo kama kitu kilichotengezwa
ili kuvutia hisia,lakini yakasema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba
bidhaa hiyo itakuwa halali chini ya sheria ya Uingereza kwa kuwa haina
kemikali yenye madhara.
CHANZO: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment