Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Ndugu Jerry Silaa
Baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri za wilaya waliosimamishwa kazi na wengine kupewa onyo kwa tuhuma za kutosimamia vyema Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wameunga mkono hatua hiyo, huku mkurugenzi wa Ilala, Isaya Mngurumi akisema onyo alilopewa lilikuwa sahihi kutokana na udhaifu uliojitokeza.
Baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri za wilaya waliosimamishwa kazi na wengine kupewa onyo kwa tuhuma za kutosimamia vyema Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wameunga mkono hatua hiyo, huku mkurugenzi wa Ilala, Isaya Mngurumi akisema onyo alilopewa lilikuwa sahihi kutokana na udhaifu uliojitokeza.
Mbali na hilo, wakurugenzi wengine wameunga mkono kusimamishwa kwao kazi, ila wakataka haki zaidi itendeke kubaini ukweli. Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wakurugenzi hao walisema kama watumishi wa umma, wanaheshimu mamlaka ya waziri.
Mngurumi alisema onyo alilopewa na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia kutokana na udhaifu
uliojitokeza kwenye uchaguzi katika halmashauri yake, lilikuwa sahihi.
Mkurugenzi huyo alisema hana pingamizi dhidi ya
hatua hiyo, kwani ni kweli dosari zilitokea ambayo ni ucheleweshwaji wa
usambazaji wa karatasi za uchaguzi zilizosababisha kuahirishwa kwa
uchaguzi huo katika mitaa 27.
“Uamuzi wa Serikali siku zote huwa ni sahihi na
nimestahili kupewa onyo, kwani hata wale waliohusika kwa upande wetu
katika udhaifu uliojitokeza tuliwawajibisha,” alisema Mngulumi. Felix Mabula wa Hanang’ alisema Kasoro katika
halmashauri yake zinahusisha ucheleweshwaji wa vifaa vya uchaguzi.
Kasoro hizo zilifanya uchaguzi huo usifanyike katika kata sita Desemba
14, mwaka huu, ingawa sasa tayari umeshafanyika.
“Binafsi naandaa taarifa ya kilichotokea hadi
kuchelewa kuanza upigaji wa kura. Nina imani Serikali na vyombo vyake
pia watafuatilia kujua tatizo lilikuwa wapi,” alisema. Hata hivyo, alisema akiwa mtumishi wa umma,
anaheshimu na kutambua mamlaka ya mwajiri wake ambaye ni waziri, hivyo
hawezi kupinga hatua iliyofikiwa juu yake.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Mbulu, Fortunatus Fwema alisema katika halmashauri hiyo
kulikuwa na matatizo katika vitongoji vitatu ambako majina yalikosewa. “Kutokana na tatizo hilo, tuliweza kuwaelimisha
wananchi na tukarudia kupiga kura siku iliyofuata na hakukuwa na
matatizo mengine,” alisema. Hata hivyo, naye alisema anaamini Serikali kupitia vyombo vyake itachunguza zaidi na kujua ukweli wa kilichotokea.
“Nina imani uchunguzi utafanyika na ukweli utajulikana, lakini
naheshimu sana uamuzi wa waziri wetu katika kuboresha utendaji kazi
wetu,” alisema. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda
mkoani Mara, Simon Mayeye amekiri kupokea barua ya kuondolewa kwenye
wadhifa huo na kueleza kuwa anakubaliana na hatua hiyo, ila yote
anamwachia Mungu.
Wakati Mayeye akisema hayo, viongozi wa vyama vya
siasa wilayani Bunda wameonyesha kusikitishwa na tukio hilo wakisema
pengine limetokana na ushindi wa kishindo waliopata wapinzani. Habari hii imeandikwa na Mussa Juma, Kelvin Matandiko, Christopher Maregesi na Pamela Chilongola, Mwananchi. Katibu Mwenezi wa Chadema jimbo la Bunda, Emmanuel
Maribwa alikielezea kitendo hicho kama uonevu, kwani anguko la CCM
katika maeneo hayo ikiwamo Halmashauri ya Mji wa Bunda ni uamuzi wa
wananchi. “Nimezipata hizo habari. Lakini kama tatizo ni
ushindi wetu (Ukawa) katika mji wa Bunda basi watakuwa wamemwonea
mkurugenzi, huu ni uamuzi wa wananchi wenyewe,” alisema Emmanuel.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment