Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
alikaririwa na vyombo vya habari jana akisema: “Rais lazima aagize
vyombo vya uchunguzi kufanya kazi yake na baada ya hapo ndipo atapata
mahali pa kuanzia,” alisema.
Hata hivyo, taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana,
ilisema Rais Kikwete ambaye alianza kazi rasmi juzi, baada ya upasuaji
aliofanyiwa mwezi uliopita, amekwishaanza kusoma Ripoti ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ripoti ya Kamati ya Bunge ya
Hesabu za Umma (PAC) na Maazimio ya Bunge kuhusu Akaunti ya Tegeta
Escrow na atayatolea uamuzi ndani ya wiki moja ijayo.
“Katika wiki moja ijayo atazitolea uamuzi kwa
maana ya kwamba yale mambo yanayomhusu yeye moja kwa moja atayatolea
uamuzi yeye, yale yanayohusu Serikali atayatolea maagizo na maelekezo ya
namna ya kuyashughulikia,” ilisema taarifa hiyo kutoka Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Kikwete
ameelekeza kuwa Ripoti ya CAG iwekwe hadharani kwa ajili ya umma kuisoma
na kujua nini hasa kimesemwa na kupendekezwa na Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Rais Kikwete ameelekeza kuwa ripoti hiyo itangazwe
kwenye magazeti yanayosomwa na watu wengi na kwenye mitandao ya
kijamii, ili iweze kupatikana kwa Watanzania wengi.
Mbali na taarifa ya CAG, Bunge lilijadili na kutoa
maazimio manane yaliyotokana na majadiliano ya PAC kuhusu uchunguzi huo
wa CAG na ule wa Takukuru.
Maazimio ya Bunge
Baada ya mjadala wa Tegeta Escrow, Bunge liliazimia kwamba:
1. Takukuru, Jeshi la Polisi na vyombo vingine
husika vya ulinzi na usalama viwachukulie hatua stahiki za kisheria, kwa
mujibu wa sheria za nchi yetu, watu wote waliotajwa na taarifa maalumu
ya kamati kuhusika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya
akaunti ya escrow na watu wengine watakaogundulika kuhusika katika
vitendo hivyo vya jinai kufuatia uchunguzi mbalimbali unaoendelea.
2. Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa
Tanesco wawajibishwe, kwa kuishauri mamlaka yao ya uteuzi kutengua
uteuzi wao.
3. Kamati husika za Kudumu za Bunge zichukue hatua
za haraka na kwa vyovyote vile kabla ya Mkutano wa 18 wa Bunge, kuwavua
nyadhifa zao wenyeviti tajwa wa kamati husika za kudumu za Bunge.
Azindua jengo Ikulu
4. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aunde Tume ya kijaji
ya uchunguzi kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya Jaji
Aloysius Mujulizi na Jaji Profesa Eudes Ruhangisa wa Mahakama Kuu ya
Tanzania
5. Serikali iandae na kuwasilisha muswada wa
marekebisho ya sheria iliyoiunda Takukuru kwa lengo la kuanzisha taasisi
mahsusi itakayoshughulikia, kupambana na kudhibiti vitendo vya rushwa
kubwa, ufisadi na hujuma za uchumi zinazotishia uhai wa taifa kiuchumi,
kijamii na kisiasa.
6. Mamlaka husika za kifedha na za kiuchunguzi,
ziitaje Stanbic Bank (Tanzania) Ltd na benki nyingine yoyote
itakayogundulika, kufuatia uchunguzi wa mamlaka za kiuchunguzi,
kujihusisha na utakatishaji wa fedha zilizotolewa katika akaunti ya
escrow, kuwa ni taasisi zenye shaka ya utakatishaji wa fedha haramu.
7. Bunge linaazimia kwamba Serikali iangalie
uwezekano wa kununua mitambo ya kufua umeme ya IPTL na kuimilikisha kwa
Tanesco kwa lengo la kuokoa fedha za shirika hilo.
8. Serikali itekeleze Azimio la Bunge la kuitaka
iwasilishe mikataba husika bungeni au kwenye Kamati zake kwa lengo la
kuliwezesha kutekeleza vyema wajibu wake wa kuisimamia na kuishauri
Serikali mapema iwezekanavyo na kwa vyovyote vile, kabla ya kumalizika
kwa Mkutano wa Bunge la Bajeti Serikali.
Azindua jengo Ikulu
Jana, Rais Kikwete alifungua jengo la shughuli
mbalimbali (multipurpose hall) la Ikulu katika moja ya shughuli zake za
kwanza baada ya kuanza kazi rasmi juzi.
Sherehe ya ufunguzi wa jengo hilo lililoko upande
wa kushoto wa bustani za Ikulu upande wa lango kuu, zilihudhuriwa na
mawaziri, makatibu makuu na viongozi waandamizi wa Serikali wakiongozwa
na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Baada ya kufungua jengo hilo lenye vyumba 53, Rais
Kikwete alitembezwa kuona shughuli zitakazofanyika. Lina ukumbi wenye
uwezo wa kubeba watu kati ya 500 na 1,000 kwa wakati mmoja.
Balozi Sefue aliyekuwa msimamizi mkuu wa ujenzi
huo, alisema ukumbi huo unaweza pia kugawanywa na kuwa tatu kubwa na
zote kutumika kwa wakati mmoja.
Jengo hilo ambalo gharama zake hazikutajwa,
limejengwa kwa maelekezo ya Rais Kikwete aliyoyatoa Dodoma Agosti 21,
2009, wakati alipoelekeza lijengwe kwa nia ya kuongeza nafasi ya
kufanyia shughuli mbalimbali Ikulu kwa kutilia maanani kuwa nafasi
imekuwa finyu kwenye jengo la sasa lililojengwa mwaka 1902.
Rais alitaka uwepo ukumbi mkubwa ili kuondokana na
gharama za kukodi wakati wa mikutano ya Ikulu ikiwamo ya viongozi wa
nchi za nje.
Balozi Sefue alizishukuru kampuni zilizohusika katika ujenzi huo; Iain Pattie Associates Ltd iliyokuwa mshauri mwelekezi; mkandarasi, kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation na mshauri wa mradi ni Wakala wa Majengo Tanzania.
CHANZO: MWANANCHI
Balozi Sefue alizishukuru kampuni zilizohusika katika ujenzi huo; Iain Pattie Associates Ltd iliyokuwa mshauri mwelekezi; mkandarasi, kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation na mshauri wa mradi ni Wakala wa Majengo Tanzania.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment