Mfanyabiashara Leonard Willoughby
aliwahi kusema; ‘siku utakayoanza kuishi kwa kuifuata mipango yako
unayopanga, kila kitu katika maisha yako kitabadilika kabisa.’
Inawezekana watu wengi wanaufahamu msemo huo, lakini Ramesh Babu
anajitapa kuyatendea kazi maneno hayo.
Babu ambaye ni kinyozi bilionea pekee nchini
India, anasema aliuchukua ushauri wa Willoughby na kuamua kuutendea kazi
tangu siku ya kwanza alipousikia na kwamba maisha yake yalianza
kubadilika.
Kwa mujibu wa Jarida la ‘Your story’ la nchini
India, Babu amefanikiwa kuvuka vizingiti kadhaa vya umaskini hadi
kufikia kuwa mmoja wa watu maarufu nchini humo akiwa na uwezo wa kununua
gari aina yoyote anayoitaka. Asema kuwa mwaka 1994 alinunua gari lake la kwanza
aina ya Maruti, lakini aliendelea na kuhifadhi fedha kidogo kidogo
alizokuwa anazipata hadi mwaka 2004, alipoanzisha kampuni ya kokodisha
magari, ikiwa na magari saba wakati huo. Hadi kufikia mwaka huu, kinyozi huyo amelinunua
magari 75 kati ya hayo matano ni ya kifahari yakiwemo, Mercedes, BMW,
Audi, mabasi kumi na lile analolipenda liitwalo Rollsw Royce. Pamoja na utajiri huo mkubwa alionao Babu, bado
anaendelea na kazi yake ya kinyozi. Akisimulia maisha yake ya awali,
anasema kuwa alizaliwa katika familia masikini, baba yake alikuwa
kinyozi na kwamba alifariki mwaka 1979 wakati Babu akiwa na miaka saba.
“Baba yangu alituachia biashara ya saluni Mtaa wa
Brigade ambalo mjomba wangu alichukua akaanza kuiongoza. Anawa anatupa
kiasi kidogo cha fedha. Tulikuwa tunakula chakula kimoja kwa siku ili
tuweze kuishi tu,” anasimulia. Anasema alipokuwa shule ya msingi, alilazimika kufanya kazi ili kuweza kujikimu kimaisha kwa kupata kiasi kidogo cha fedha.
“Nilikuwa nikibeba magazeti na chupa za maziwa na
kitu kingine chochote ambacho kingeweza kupunguza ugumu wa maisha ya
mama yangu. Hii ndiyo sababu ya kuhitimu masomo yangu,” anasema.
Baadaye alifanikiwa uendelea na masomo yake, jambo
lililomfanya mama yake aanzishe ugomvi na mjomba aliyekuwa akisimamia
duka baada ya kugoma kutoa fedha za matumizi.
“Ndipo nilipomwambia mama nitachukua saluni na
kukiendesha mwenyewe. Hakupenda uamuzi huo kwa kuwa alifikiri nitaacha
masomo, lakini nilianza kazi hiyo. “Asubuhi nilikuwa saluni, jioni nilikwenda
masomoni kisha usiku nilikuwa saluni tena na kufanya kazi hadi saa 7
usiku. Hivyo ndivyo nilivyoanza kuitwa kinyozi,” anasema.
Milango ya baraka inafunguka
Mwishoni mwa mwaka 1993, Babu alinunua gari la
mtumba aina ya Maruti Van. Kwa kuwa mjomba wangu alikuwa ameshanunua
gari moja alinishawishi na mimi kununua.ilibidi babu yangu aweke nyumba
yake dhamana nini nimchukue mkopo. “Binti katika nyumba ambayo mama yangu alikuwa
akifanya kazi, aliniuliza kwa nini sikodishi gari badala yake naliegesha
tu nyumbani. Alinifundisha namna ya kusimamia biashara hiyo, kwangu
alikuwa kama dada yangu,” anasimulia.
Kuanzia mwaka 1994 ndipo Babu alipojiingiza rasmi
kwenye biashara ya kukodisha magari. Magari ya kwanza niliyapata katika
Kampuni ya Intel, alikokuwa anafanya kazi Nandini Akka.
“Taratibu nilianza kuongeza magari kwenye yadi
yangu. Kufikia mwaka 2004 nilikuwa na magari sita tu, biashara ilikuwa
haifanyi vizuri kutokana na ushindani mkali uliokuwapo. “Kwa sababu kila mtu alikuwa na magari madogo ya kawaida, nilitaka ninunue magari ya kifahari kupunguza ushindani,” anasema.
Babu anasema siku aliponunua gari lake la kwanza
la kifahari mwaka 2004, kila mtu alimwambia kuwa amefanya kosa kubwa.
Niliogopa lakini sikuwa na namna zaidi ya kuendelea na mpango wangu.
“Nilijiambiwa mwenyewe kuwa ningeuza magari kama
hali ingekuwa mbaya. Bahati nzuri kwangu biashara ililipa sana. Nilikuwa
mtu wa kwanza katika Bangalore yote kuagiza magari ya kifahari mapya,”
anasema.
Babu anasema kama unataka kufanya biashara lazima
uwe tayari kukabiliana ana hatari yoyote itakayojitokeza, wakati
akinunua Rolls Royce mwaka 2011 rafiki zake walimwonya kuwa anacheza
‘kamali’ na biashara yake. “Niliwaambia nilishajitosa mwaka 2004, kwa nini
nisijaribu tena miaka kumi baadaye? Ilinigharibu fedha nyingi, lakini
kama ilivyokuwa mwanzo biashara ililipa sana” anasema.
Changamoto
Changamoto kubwa kwake ni gharama za kulipa kodi ya ushuru wa barabara, kiasi kwamba sijui jambo hilo nilifanyaje. Babu asema mwanzoni wakati anaanza kufanya biashara ya magari
alikuwa akilipa kodi kila baada ya miezi minne, lakini sasa atalazimika
kubadili utaratibu huo kwa kuwa kodi zimekuwa kubwa mno kiasi kwamba
zinaweza ‘kumvurugia’ mpango wake wa kununua magari ya Limousines na
mengine ya kifahari mwaka 2015. Babu anawaambia watu wanaotaka kuwa kama yeye: “Fanya kazi kwa bidii, kuwa mcheshi, mambo mengine yanayobaki ni bahati tu.”
Kuhusu ndoa yake
CHANZO: MWANANCHI
Kuhusu ndoa yake
Babu ameoa na ana watoto watatu, wote wakiwa ni wanafunzi. Watoto wawili wa kwanza ni wasichana, mtoto wa mwisho ni mvulana. “Nitawafundisha watoto wangu kufanya kazi zangu zote mbili (kunyoa na kukodisha magari),” anasema Babu.
Babu anasifika kwa kutokuwa mwanachama wa klabu yoyote kwa kile anachosema kuwa hana nafasi ya kujihusisha na mambo hayo. Kinyozi huyo hupenda kuitumia Jumapili yote katika saluni yake, jambo linalomaanisha kuwa hana kitu anachokiita ‘mapumziko’. Amewahi kusafiri kwenda Ujerumani kama mtalii na Singapore kwa ajili ya kwenda kujifunza kunyoa nywele za wanawake.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment