Nyumba tisa zimeteketezwa kwa moto katika kisiwa cha
Tumbatu Kaskazini Unguja muda mfupi baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) kutangaza ushindi wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.
Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, baadhi ya wafuasi na wanachama wa CCM kisiwani hapo walianza kushangilia ushindi huo. Hata hivyo, wakati wakiendelea kushangilia ushindi huo huku wakilidhihaki kundi lingine hali iliyosababisha warushiane mawe na mwishowe kuchomeana nyumba hizo.
Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, baadhi ya wafuasi na wanachama wa CCM kisiwani hapo walianza kushangilia ushindi huo. Hata hivyo, wakati wakiendelea kushangilia ushindi huo huku wakilidhihaki kundi lingine hali iliyosababisha warushiane mawe na mwishowe kuchomeana nyumba hizo.
Akizungumza na Nipashe, mmoja wa wananchi wa kisiwa hicho, Juma
Ali, alisema kuwa wafuasi wa CCM waliokuwa wakisherehekea ushindi
walikuwa wakiwazomea wafuasi wa wanaoaminika kuwa ni wa chama kingine na
kuanza kupigana.
Alisema ugomvi huo ulizusha taharuki hadi kufikia wafuasi hao wa
pande mbili kuanza kurushiana mawe hadi kuchomeana moto nyumba zao za
makaazi yao.
“Kwa kweli hali ilikuwa mbaya katika kisiwa hiki cha Tumbatu hasa
kijiji cha Tumbatu Gomani ambacho kina wafuasi wengi wa CCM na kijiji
cha Tumbatu Chwaka ambacho kina wafuasi wengi wa chama kingine,”
alisema. Alifafanua kuwa nyumba zilizochomwa moto ni za Gomani na
Chwaka.
Kamishana wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame, alisema
jumla ya nyumba tisa katika kisiwa hicho zimechomwa moto na chanzo cha
ugomvi huo ni matokeo ya mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia CCM.
Alisema tayari polisi kwa kushirikiana na vikosi vya SMZ,
vimeshatuliza ghasia hizo kisiwani humo na pia wanaendelea kufanya
uchunguzi ili kubaini waliohusika na vitendo hivyo vya uvunjifu wa
amani.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment