Maonyesho ya 10 ya biashara kwa nchi za Afrika
Mashariki yaliyoandaliwa na Kituo cha Biashara, Viwanda na Kilimo Nchini
(TCCIA) Kanda ya Mwanza (TCCIA), yamedorora kutokana na kukumbwa na
changamoto mbalimbali.
Yakiwa yameingia siku ya sita sasa, maonyesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya Chuo cha Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) jijini Mwanza, yanashirikisha nchi zote za Afrika Mashariki isipokuwa Burundi.
Mashindano hayo yalianza tangu Agosti 28 na yanatarajiwa kumalizika Septemba 9, mwaka huu, huku yakiwa na washiriki 165.
Akizungumza na Nipashe jana, Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mwanza,
Elibariki Mmari, alisema maonyesho hayo yanakabiliwa na changamoto
mbalimbali zikiwamo za muitikio mdogo wa washiriki na wakazi wa jiji la
Mwanza kulalamikia umbali yanakofanyikia.
Aidha, Mmari alisema usalama wa washiriki umekuwa mdogo kutokana na
kimbunga kiliinua mahema manane na kuwajeruhi vibaya washiriki wanne,
hivyo kulazimika TCCIA kuingia gharama za kuwatibu majeruhi.
Mmari alisema baadhi ya washiriki kutoka Uganda na bidhaa zao,
walikamatwa katika mpaka wa Tanzania na Uganda wa Mutukula, hivyo
kulazimika kushikiliwa kwa siku nne. “Tunaitupia lawama idara ya mapato na ukaguzi mipakani kwa
kuchelewesha kutatua tatizo hilo…tusiwakatishe tamaa washiriki na kisha
kuyakimbia maonyesho haya,” alisema Mmari.
Kwa upande wa washiriki wa maonyesho hayo, waliponda maandalizi
duni yaliyofanywa na TCCIA kwa sababu siku tatu kabla walikuwa
hawajakamilisha maandalizi ya mabanda na kukiuka makubaliano licha ya
kulipa fedha mapema.
Sauda Mninga, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saka asali and
partners ya mkoani Dodoma, aliilaumu TCCIA kwa tozo yake ya mlangoni kwa
wateja (wananchi) wanaokuja kushuhudia maonyesho hayo na kuchochea
idadi ndogo ya watu wanaohudhuria.
“Tunawaomba waandaaji wawaruhusu watu waingie bure ili kuleta
hamasa ya maonyesho haya na kuongeza idadi ya mahudhurio, kitendo cha
kuwatoza wananchi wakiwamo watoto kinasababisha kudorora kwa maonyesho
haya,” alisema Mninga.
Hata hivyo, Mmari alitoa sababu ya kudorora kwa maonyesho hayo kuwa
ni kitendo cha kuhama hama kila mwaka kutokana na TCCIA kutopata.
CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment