Pages

Wednesday, September 02, 2015

KAMPENI KUHAMASISHA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Taasisi ya kueneza amani nchini ya Global Peace Foundation (GPFTZ) kwa kushirikiana na Baraza la Wadhamini la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT) imezindua kampeni ya kuhamasisha amani katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa IRCPT, Lanon Godela, alisema lengo la kampeni hiyo ni kuhamasisha wananchi kushiriki uchaguzi huo kwa amani na utulivu.
Alisema katika mkakati wao wa uhamasishaji wamelenga zaidi makundi ya vijana kwa kuwa ndiyo wengi zaidi ikilinganishwa na makundi mengine na pia ndilo ambalo limekuwa likishawishika  kuingia katika viashiria vya kuingia katika machafuko.
Kundi jingine alisema ni la wanawake ambao wamekuwa waathirika wakubwa katika nchi mbalimbali duniani pale yanapotokea machafuko.
Godela alisema kazi kubwa ya kampeni hiyo ni kuwaelimisha wananchi faida za kushiriki katika uchaguzi kwa amani  pasipo kuangalia vyama vya siasa wanavyotoka bali kuliweka mbele taifa na maslahi yake.
“Kampeni hii imeandaliwa maalum kwa ajili ya kuhamasisha wanawake na vijana kuwa mabalozi wazuri wa kulinda na kuitetea amani ya nchi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu,  tunaamini wakipata elimu watajiepusha na vitendo mbalimbali vya uchochezi na uharibifu wa amani ya nchi,” alisema.
Godela alisema katika kufanikisha hilo, pia wamepanga kuyafikia makundi hayo kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment