Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Hivi karibuni nimesaidiana kimawazo na
Watanzania wenzangu katika kufanya uchambuzi wa watu wanaotajwa au
waliojitangaza kuwa watawania uteule wa urais kupitia CCM na nalishukuru
gazeti hili kwa kukubali kuchapisha maoni yangu.
Haikuwa kazi nyepesi na namshukuru kila mmoja
aliyetoa mchango wake wa mawazo na aliyefuatilia nilichoandika, lakini
nawaomba radhi wale wote ambao hawakupenda nilivyoandika na hasa
walioumizwa lakini mrejesho mkubwa niliopokea kutoka kwa jamii ni
kuendelea kuifanya kazi hii kwa sababu ina tija kwa Taifa.
Kabla sijafunga ukurasa wa CCM na kuhamia kwa
vyama vya upinzani niliona nimalizie na kidokezo cha mwisho cha
uchambuzi mfupi wa fikra zangu juu ya nani anaweza kupitishwa na CCM
kuwa mgombea na huenda Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa
chama hicho kitashinda uchaguzi wa mwaka huu.
Kwa kifupi nitajadili nanyi sifa kumi za mtu huyo
kutokana na dalili na mwelekeo wa CCM, hali inayokabiliwa nayo hivi sasa
na mpasuko unaoinyemelea.
1. Anayeelewana na kukubalika kwa Rais anayemaliza muda wake
Watu wengi niliozungumza nao wanaidharau sifa hii.
Lakini bado naona kuwa CCM itaitumia kumpata mgombea. Watu wengi
walijaribu kuniambia kuwa hata mwaka 1995, Benjamin Mkapa hakuwa chaguo
la Ali Hassan Mwinyi na kwamba hata mwaka 2005, Jakaya Kikwete hakuwa
chaguo la Mkapa na kwamba mwaka 2010 pia Kikwete hatapata chaguo lake.
Lakini nasisitiza kuwa nyakati zinabadilika sana
na huenda CCM ikapitisha mgombea ambaye anaweza kuwa chaguo la Kikwete
kwani Rais huyo anaifahamu CCM vizuri na amefanya mambo mengi katika
siasa za chama hicho.
Hatari ya sifa hii
Chama kinapopitisha mgombea kwa sababu tu
anafahamiana na kukubalika na kiongozi anayemaliza muda wake, huwa kuna
hatari ya mpasuko mkubwa ikiwa wagombea wengine hawataridhishwa na
upendeleo aliopewa mwenzao na hivyo wanaweza kufanya uamuzi wa kuondoka
katika chama hicho.
2. Mchapakazi na mwadilifu lakini atakayekubali kusikiliza mahitaji na matakwa ya CCM
CCM inahitaji mgombea mchapakazi na mwadilifu ili
kuziba baadhi ya mashimo yaliyoachwa na Serikali inayoondoka kwa haraka
na lengo la kufanya hivi ni kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea
kukiamini na labda kukiunga mkono. Lakini CCM ya sasa bado inahitaji
sana msaada wa Dola ili iendelee kuwa madarakani. Kuna wakati Rais
Kikwete mwenyewe aliwahi kuwatamkia wana CCM kuwa wanafanya kazi kwa
kutaka kusaidiwa na vyombo vya dola.
Hatari za sifa hii
3. Aliyekulia katika chama na anakijua vizuri
4. Mzoefu wa kufanya kazi nchini
5. Asiye na makundi na anayejua mahitaji ya makundi yanayosigana
Hatari iliyopo ni uendelezaji wa mambo yaleyale ambayo
yamekikumba chama hicho kwa miongo kadhaa iliyopita. CCM inahitaji mtu
mwadilifu, mchapakazi na ambaye atakataa kabisa kusikiliza matakwa ya
chama chake ili ajenge uchumi imara wa nchi, nidhamu kwa watendaji wa
Serikali na kusimamia maendeleo ya Taifa huku akiweka “Taifa Mbele na
chama baadaye”. Mgombea wa CCM ambaye atakesha akitekeleza matakwa ya
CCM hatakuwa tofauti na wenzake kadhaa waliopita.
3. Aliyekulia katika chama na anakijua vizuri
Naiona CCM ikimpitisha mgombea ambaye anakijua
vizuri chama hicho na hasa aliyekulia ndani ya chama ikiamini kuwa
atakuwa na uwezo mzuri wa kupambana na kuzikabili changamoto za kichama
na za kiserikali huku akijua anachokifanya kwa masilahi ya chama na
serikali.
Hatari ya sifa hii
Katika dunia ya leo ambayo vyama vinavyoendelea
vinajaribu pia kutenganisha mamlaka ya kichama na kiserikali na hata
kuwa na watu tofauti katika uongozi wa nchi na ule wa chama, sifa hii
inajimaliza yenyewe.
Kwa sababu watu waliokulia ndani ya chama hicho
ndiyo wamekuwa wakijenga makundi makubwa, kujuana, kupendeleana na
kufumbiana macho, ukiniuliza nitasema CCM ya sasa inahitaji mtu
“atakayekuwa anamuua nyani kwa kumfumbia macho”.
Yaani CCM inahitaji mtu asiyekulia ndani ya chama
hicho na asiyejua ‘uhafidhina’, ‘uswahili’ wa wanaojiita “wenye chama”.
Kwa lugha ya mtaani, chama hicho kinahitaji ‘mgombea kauzu’ na anayeweza
kusimamia mambo ya nchi kwa matakwa ya raia bila kuyumbishwa na matakwa
ya chama hicho, kama hayana tija. Mtu wa namna hii hawezi kuwa
aliyekulia ndani ya CCM.
4. Mzoefu wa kufanya kazi nchini
Naiona sifa hii kama muhimu kwa CCM na isiyo na
hatari kubwa. Kwamba inaweza kumteua mgombea mwenye uzoefu mkubwa katika
kufanya kazi serikalini lakini awe anakijua chama hicho vizuri. Mtu wa
namna hii anaweza kuwa na tija kwa chama hicho hasa ikiwa rekodi zake za
utumishi ni nzuri na zenye tija.
5. Asiye na makundi na anayejua mahitaji ya makundi yanayosigana
Natambua kuwa tunakubaliana CCM iko kwenye mpasuko
unaotokana na makundi na chama hicho hakina namna ya kufanya zaidi ya
kuteua mgombea asiye na makundi na ambaye atakubaliwa na makundi mengine
lakini ambaye ikiwa atachaguliwa, ataweza kuyalea makundi hayo kwa
sababu anajua mahitaji yao na labda ataweza kutoa mahitaji ya makundi
hayo ili kuyafanya yatulie na kutoisumbua Serikali na chama hicho.
Katika dhana hii ndipo wale wagombea ‘neutral’ huingia na kupata fursa ya kutuliza hali ya mambo.
Hatari ya sifa hii
Mgombea atakayeteuliwa kwa dhana ya kuwa ‘neutral’
anaweza kuwa hasimu mkubwa wa moja ya makundi yanayosigana na mapambano
ya kutomuunga mkono yakaendelea. Au, mtu huyo atakayeteuliwa anaweza
kuwa dhaifu kimtandao na kiuwezo kuliko yalivyo makundi yanayopambana.
Kitakachojitokeza ni mpasuko mkubwa zaidi kuliko ambao ulikuwa
unatatuliwa na huu wa pili unaweza kabisa kukosa mtu wa kuutatua. Kwa
mtazamo wangu CCM, ilihitaji mgombea ambaye akiingia atasambaratisha
makundi yote na labda kukiacha chama hicho ‘kipumue’.
6. Anayeweza kukemea rushwa huku akiilinda CCM
Naweza kuthubutu kusema kuwa tangu alipoondoka
Mwalimu Nyerere, CCM haijawahi kupata mgombea na hata kiongozi wa nchi
aliyeonyesha nia ya dhati, moyo, malengo, kiu na uwazi katika mapambano
dhidi ya rushwa. Moja ya mambo ambayo yanakiweka chama hicho kwenye hali
mbaya kisiasa mwaka huu ni tuhuma kubwa za rushwa na ufisadi.
Hakika hapa ndipo CCM ilipo na mtihani mgumu
zaidi, kwamba inaipasa kuteua mgombea msafi sana na asiye na madoa na
ambaye anaichukia rushwa kuliko kifo na ameonyesha uwezo wa kupambana na
rushwa katika rekodi zake, maneno yake na vitendo vyake.
Hatari ya sifa hii
CCM inapaswa kuita ‘nyeusi kama nyeusi na nyeupe
vivyo hivyo’ kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. Huu ni uchaguzi wa
uamuzi pia na wa kuleta mapinduzi makubwa katika nchi na ushindani
mkubwa kupita wakati wowote ule. Huu si mwaka wa kutaka mgombea
mwadilifu na mpambanaji wa rushwa na wakati huohuo kutaka akilinde chama
chake. CCM inahitaji mgombea ambaye atakuwa tayari hata kurudisha kadi
ya CCM ikiwa chama chake kitaonekana kinaendekeza mtindo wa kutaka
kulindwa kwa watu wake na kwa chama katika tuhuma kubwa za ufisadi na
rushwa. Kufanya kinyume na hapo kutaendeleza yaleyale yaliyowakatisha
Watanzania tamaa kwa miongo kadhaa iliyopita na adhabu yake kwa mwaka
huu inaweza kuwa kubwa.
7. Maarufu, anayekubalika na anayeweza kuwa mshindi
CCM itahitaji mgombea ambaye yeye mwenyewe pia ni
mtaji tosha wa kupata kura. Mwaka 2005 wakati chama hicho kilikuwa
taabani kisiasa, kilikuja kuamshwa na nguvu, umaarufu na kukubalika kwa
Jakaya Kikwete, kikajiandaa na ushindi wa kimbunga pamoja na kwamba
kilisaidiwa sana na mifumo ya dola. Mwaka huu pia nadhani CCM itahitaji
mtu wa namna hiyo ‘kama yupo’ ili kukiokoa. Maana ukizunguka vijijini
unaona wananchi walivyochoka na wanavyohitaji mabadiliko.
Hatari za sifa hii
Kuteua mgombea maarufu kuliko chama kuna faida tu
wakati wa kupiga kura na kushinda. Mara nyingi hakuna faida wakati wa
kutekeleza ajenda za chama na kuwaletea maendeleo wananchi.
8. Mwenye umri wa kati, msomi, mtulivu/mpole na mwenye busara
Sote tunakubaliana kuwa miaka 10 ya Kikwete imekuwa ya suluba
kubwa, kwa mara ya kwanza tumeshuhudia (hasa miaka yake mitano ya
mwisho), nchi ikishindwa kutekeleza baadhi ya bajeti za wizara kwa
asilimia 50, fedha za miradi ya maendeleo zikitolewa kwa asilimia hadi
30 au 40 huku asilimia 70 hadi 60 zikikosekana katika miradi mingi,
kuporomoka kwa uchumi, kuporomoka kwa shilingi na mambo mengine.
Inawezekana kuwa miaka 10 iliyopita Watanzania
walichagua mtu maarufu na anayekubalika lakini hawakuangalia ana uwezo
kiasi gani kuondoa umaskini, kuleta maendeleo, kurudisha nidhamu na
uwajibikaji serikalini na kulinda kazi za raia. Kwa hiyo, yanayotokea
leo, huenda ni madhara ya kuchagua mtu maarufu bila kuangalia umaarufu
ule una tija gani kwa maendeleo na mahitaji ya Taifa.
8. Mwenye umri wa kati, msomi, mtulivu/mpole na mwenye busara
Katika kuweka hali ya mambo sawa, huenda CCM
ikateua mgombea kwa sababu ya sifa hizi. Mtu wa umri wa kati ili
kuwavutia vijana, wanawake na wazee (makundi yote ya kijamii) na katika
chaguzi nyingine zote za nyuma CCM ilipitisha wagombea wake wakiwa na
umri wa kati (chini ya miaka 60) na kufanikiwa.
Lakini pia, CCM inaweza kupitisha mgombea msomi
ili aendane na kasi ya utendaji ya mabadiliko ya dunia na kuweza
kuanzisha uongozi wa kisasa. Mahitaji ya kiongozi mwenye busara
yanatokana na sababu kuwa nchi hii ni kubwa (Tanzania inalingana na nchi
zote za Ulaya Magharibi, zikiwekwa pamoja).
Hii ni nchi yenye changamoto nyingi na viashiria
vya migogoro vinavyoshika kasi. Inahitaji mtu mwenye busara za kutosha
kuweza kuipeleka mbele.
Hatari ya sifa hii
Pamoja na mahitaji ya kiongozi mtulivu na mwenye
busara, kiongozi huyo anapaswa asiwe mpole hata kidogo. Taifa letu
lilipofika linahitaji rais mwenye sifa zozote zile lakini lazima awe
mkali kama pilipili pale watendaji wanapojaribu kupindisha mambo fulani.
Asiishie tu kuwa mkali, pia achukue hatua stahiki
kila mambo yanapoborongwa. Watu wengi ambao tunaambiwa wana busara kila
nikiwaangalia nawaona kama wapole. Inawezekana kabisa kuwa Watanzania
wengi wanaona kama busara na upole ni vitu vinavyokwenda pamoja.
Watu wapole wana matatizo makubwa katika usimamizi
na kwa hakika binadamu anapaswa awe mpole katika mazingira yanayohitaji
upole lakini awe mkali katika mazingira yanayohitaji ukali wa kiwango
hichohicho.
9. Anayeweza kuupigania Muungano wa Serikali mbili kwa dhati
9. Anayeweza kuupigania Muungano wa Serikali mbili kwa dhati
Sifa hii nayo isidharauliwe. Kwamba CCM
itaitegemea katika kumpata mgombea urais wake. Tukumbuke kuwa CCM
haiwakubali na kuwaamini viongozi wanaotaka Muungano nje ya mfumo wa
Serikali mbili. Ndiyo kusema kuwa CCM kwenye suala la Muungano haitaki
mjadala na haitaki wananchi wajiamulie wanataka wa namna gani.
10. Mwenye uzoefu na masuala ya kimataifa
Hitimisho:
Nasisitiza kuwa CCM inamtaka mtu ambaye anataka Muungano wa
serikali mbili uendelee na si kinyume na hapo. Hii ni sera ya CCM na
inaamini kuwa lazima iendelee kutekelezwa na wananchi wote tena bila
kujali kuwa nchi hii sasa ina vyama vingi.
Hatari ya sifa hii
Kitakachojitokeza ni kuwa, wananchi wengi
wanaotaka kuwe na mjadala wa kitaifa wa muundo wa muungano wataendelea
kudhibitiwa na hata kuonekana kama maadui wa Taifa kwa jambo la
kimtizamo tu.
Kama nchi itatumia nguvu nyingi, akili nyingi na
kila rasilimali kupigania mfumo wa serikali mbili na kusahau kuwa
mahitaji makubwa ya wananchi ni maendeleo, naona CCM itazidi kushuka
thamani na kupoteza mwelekeo. Kwa maoni yangu, CCM ingesaidiwa zaidi na
mgombea ambaye atakuja na mtazamo huru juu ya muungano, hasa yule ambaye
atakuwa tayari kuanzisha mjadala wa kitaifa ili wananchi waamue
wanataka muungano wa namna gani.
Lakini pia, kuwaacha wagombea ambao wana sifa
kubwa kuongoza nchi eti kwa sababu tu hawaamini sana katika serikali
mbili itakuwa ni makosa makubwa. Sababu hii inaweza kukifanya chama
hicho kichague mgombea mbovu kwa sababu atalinda serikali mbili.
10. Mwenye uzoefu na masuala ya kimataifa
Kwamba kwa namna dunia ilivyokumbwa na
migawanyiko, mitanzuko na hata mabadiliko makubwa ya kidiplomasia,
huenda CCM ikahitaji mtu mwenye uzoefu mkubwa wa masuala ya kimataifa
kwa ngazi na kiwango ambacho chama hicho kitaona inafaa. Lengo litakuwa
ni kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kufanya vizuri, kuheshimika na
kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.
Hatari ya sifa hii
Watu wengi waliobobea katika masuala ya kimataifa
na kidiplomasia huamini katika dhana ya kushughulika kimataifa, kusafiri
sana, kusaka misaada na marafiki kimataifa n.k. Ndiyo maana serikali
inayomaliza muda wake imetumia muda mkubwa kufanya masuala ya kimataifa
lakini hadi naindikapo hali ya nchi kimaendelea, kiuchumi na kijamii
ndiyo kwanza inazidi kuwa mbaya.
Nadhani Taifa la Tanzania ya sasa linahitaji mtu
mweledi wa kiwango cha kutosha kuweza kuongoza nchi na ambaye atakuwa na
uwezo mkubwa zaidi katika kutengeneza fursa pana za kiuchumi ndani ya
nchi, ambaye ataweza kuhamasisha wafanyabiashara wa ndani ya nchi
wawekeze katika viwanda vidogovidgo na Serikali iwasaidie kusimamia
sehemu ya mitaji ya viwanda vikubwa. Taifa linahitaji mtu ambaye
atatumia muda wake mwingi akiwa mikoani na ofisini akisimamia
utekelezaji wa maendeleo ya nchi yeye mwenyewe kuliko kusafiri kila
uchwao kwenda nje ya nchi.
Kwa mtizamo wangu, kubobea katika masuala ya
kimataifa huku ukikosa weledi muhimu wa namna ya kupandisha uchumi wa
Taifa na wananchi ukiwa hapahapa ndani – hakuna tija yoyote katika Taifa
maskini kama Tanzania.
Hitimisho:
Huu ni mwaka wa kusuka au kunyoa kwa CCM, chama hicho kikongwe
huenda kinakabiliwa na changamoto kubwa kuliko wakati wowote ule
kihistoria. Nguvu ya vyama vya upinzani imekuwa kubwa na haina mfano.
Makosa ya CCM katika uteuzi wake ni jambo muhimu kwa vyama vya upinzani
na ni suala la kujutia kwa CCM.
Sifa za mgombea wa CCM zina maana kubwa kama
karata ya kutafuta ushindi wa chama hicho, na naamini kuwa kwa mwaka
huu, kama CCM itaondoka madarakani, basi sababu mojawapo inaweza kuwa
aina ya mgombea iliyempitisha.
Hata hivyo, nawatakia wana CCM na Watanzania wote
tafakuri nzito juu ya mteule wake ambaye lazima tuseme ukweli kuwa,
ikiwa atashinda uchaguzi, ndiye atakuwa Rais wetu wa awamu ya tano.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment