“Simfanyii mtu kampeni, ninachosema ni kwamba, mambo hayajakamilika na
tunataka yakamilike na michakato yote aliyeianzisha ni Rais Kikwete, ni
vyema akaimaliza,”
Augustino Mrema.
Mbunge wa Vunjo,
Augustine Mrema ametajwa kuwa ni mpinzani mstaarabu kwa sababu ya kuweka
kando itikadi za kisiasa na kushirikiana na Serikali ya Chama cha
Mapinduzi (CCM), kutekeleza shughuli za maendeleo.
Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Taifa wa
Umoja wa Vijana wa CCM, (UVCCM), Sadifa Juma alisema anampongeza Mrema
kwa uamuzi wake ambao umeonyesha ukomavu mkubwa wa kisiasa katika
kuwatumikia wananchi.
Sadifa aliyasema hayo jana alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro juzi. Sadifa yuko katika ziara ya kikazi ya kuimarisha
jumuiya hiyo pamoja na chama kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu mkoani
Kilimanjaro.
Hata hivyo, alisema licha ya Mrema kufanya kazi kubwa ya kuwatumikia wananchi, kwa sasa kiongozi huyo anapaswa kupumzika.
Kuhusu nafasi ya vijana katika uongozi, Sadifa
alisema licha ya jumuiya hiyo kupigania vijana kushiriki katika Uchaguzi
Mkuu mwaka huu, hatakubali kuona jumuiya na chama kinatoa fursa hiyo
kwa vijana wasio na uwezo na wanaoweza kukiletea matokeo mabaya chama
hicho.
Awali, Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Kilimanjaro,
Fred Mushi alisema jumuiya hiyo imeanza kutekeleza mipango inayolenga
kukiimarisha chama chao ili kipate ushindi wa kishindo katika Uchaguzi
Mkuu ujao. Katibu wa UVCCM mkoani hapa, Yasin Lema aliwaonya vijana kuacha ushabiki wa kisiasa usio na manufaa kwao.
CHANZO: MWANACHI

No comments:
Post a Comment