Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.
Kuna kila dalili kwamba
Chadema na vyama washirika vina mpango wa kumsimamisha Katibu Mkuu wa
Chadema, Dk Willibrod Slaa kugombea urais Oktoba mwaka huu.
Dalili hizo zilijitokeza hadharani juzi kutokana
na kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu aliyoitoa katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Majengo, Moshi
akimtaja Dk Slaa kama ndiye rais ajaye huku akieleza uwezekano wa Ukawa
kuchukua nchi.
Lissu alimtaja Dk Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini,
Philemon Ndesamburo kuwa ndiyo wabunge wa Chadema ambao hawajawahi
kushindwa na CCM tangu mwaka 1995.
“Historia hiyo itasema mbunge mmoja kati yao
(ambao hawajawahi kushindwa na CCM) ni Mzee Ndesamburo na historia hiyo
itasema mbunge wa pili ambaye hajawahi kushindwa na CCM ni Dk Willibrod
Slaa, rais wetu ajaye,” alisema Lissu.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu (CC) ya Chadema, alisema
katika historia ya Taifa hili kuna uwezekano mkubwa wa Chadema na vyama
washirika kuingia Ikulu baada ya Oktoba.
Vyama washirika ambavyo vinaunda Umoja wa Katiba
ya Wananchi (Ukawa) vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, vimepanga
kusimamisha mgombea mmoja katika ngazi zote za uchaguzi kuanzia urais
hadi udiwani katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Dk Slaa aligombea urais 2010 na kushika nafasi ya
pili kwa kupata kura milioni 2.3 sawa na asilimia 26.34 nyuma ya Rais
Jakaya Kikwete aliyeshinda kwa kura milioni 5.3 sawa na asilimia 61.17.
Hadi sasa Ukawa haijateua wagombea wake katika
ngazi hizo ambazo ni urais, ubunge na udiwani ambao watachuana na
wagombea wa vyama vingine.
Katika mkutano
Katika hotuba yake hiyo, Lissu alisema: “Katika
miaka 20 ya kwanza ya mfumo wa vyama vingi, kuna wabunge wawili pekee
ambao hawajawahi kushindwa na CCM.”
Kauli hiyo ya Lissu iliwafanya wananchi hao kulipuka kwa furaha na kukatisha hotuba hiyo.
Hata hivyo, Lissu hakufafanua zaidi kuhusu kauli
yake hiyo zaidi ya kusisitiza kuwa Watanzania wanapaswa kuenzi mchango
wa kiongozi huyo na wa Ndesamburo.
Ukawa kuchukua nchi
Fitina kupenyezwa
Ukawa kuchukua nchi
Lissu alisema mwaka huu kwa mara ya kwanza katika
historia ya nchi, kuna uwezekano mkubwa kwa Chadema na vyama washirika
wa Ukawa kushinda uchaguzi na kuchukua nchi.
“Kuna uwezekano mkubwa (kushinda urais) na kwa
sababu hiyo kuna uwezekano mkubwa vilevile kwa yeyote atakayeteuliwa
kugombea udiwani au ubunge kushinda uchaguzi,” alisema Lissu na
kuongeza:
“Uwezekano huo ni mkubwa kuliko kipindi chochote
cha miaka 20 ya mfumo wa vyama vingi. Upo uwezekano wa kuwa na wabunge
wengi kila mahali. Upo uwezekano mkubwa wa kuunda Serikali.”
Fitina kupenyezwa
Hata hivyo, Lissu alitahadharisha kuwa kutokana na
uwezekano huo mkubwa wa Ukawa kuchukua nchi, pia ni kipindi mwafaka cha
CCM kupenyeza fitina na majungu ili kufarakanisha umoja huo.
“Kwa sababu ya uwezekano huo huu ndiyo wakati
mwafaka wa fitina na majungu na watu kupenyeza vipande 30 vya fedha
(rushwa). Huu ndiyo wakati kwa watu kutaka uongozi kwa rushwa,” alisema.
Lissu alifafanua miaka ya nyuma chama hicho
kilikuwa kikipata shida ya kupata wagombea lakini kwa kuwa sasa baadhi
ya majimbo yana wagombea zaidi ya watano kwa sababu kuna matumaini
mbele.
“Kuna majimbo Kanda ya Ziwa yana wagombea 18 kwa
sababu kwa mara ya kwanza watu wanaona kuna tumaini. Watu wanaona hiki
chama na washirika wake wa Ukawa ni vyama vya kwenda Ikulu.”
“Kwa hiyo kila mtu anataka awe mbunge na kila mtu
anataka awe waziri. Ukiwa mbunge uwezekano wa kuwa waziri ni mkubwa. Kwa
hiyo ni kipindi cha fitina. Ndiyo kipindi cha majungu,” alisema.
Lissu alitahadharisha kuwa kama viongozi na
wanachama wataruhusu hali hiyo itokee ni wazi kuwa Ukawa itaparanganyika
na kutoa mwanya kwa CCM kuchukua tena dola.
“Tukifarakana nchi itarudi kwa watu wa Escrow,
Epa, Tokomeza na watu wa aina hiyo. Hiki ni kipindi cha kuhakikisha
wagombea wetu wote wanakuwa na nidhamu,” alisema Lissu na kuongeza:
Ndesamburo na meya
“Kamati Kuu yetu (Chadema), imesema tuna majimbo 24 tuliyoyapata
2010. Haya majimbo tunahitaji kuyalinda kwa udi na uvumba. Kamati Kuu
imesema haitaruhusu ugomvi na fitina katika majimbo haya.”
Alisema kama chama hicho kitaruhusu kila anayetaka
kugombea ubunge katika majimbo hayo afanye anavyotaka, upo uwezekano wa
kuyapoteza jambo ambalo hawako tayari nalo.
Lissu alitumia mkutano huo kutoa somo wanaotaka
kurithi mikoba ya Ndesamburo akisema kunahitajika nidhamu ya hali ya
juu, “hivi ni kweli hivi ‘vimiguu’ vyangu vinaweza kuvaa viatu vya
Ndesa?”
Ndesamburo na meya
Kwa upande wake, Ndesamburo alitumia mkutano huo
kueleza kuwa alipomtangaza Meya wa Manispaa ya Moshi, Jaffar Michael
kuwa mrithi wake hakuvunja katiba wala kanuni za chama chake.
“Niliposema sipiganii, nikasema kuna kijana
nimemjenga sikufanya masihara. Wala sijavunja kanuni wala katiba ya
chama,” alisema Ndesamburo huku akishangiliwa na kuongeza: “Kila mmoja
ana haki ya kusema huyu anafaa. Mwenye ubavu aje akashindane na mtu
ambaye Ndesamburo amesema anafaa.”
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment