Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo alipokuwa akiangalia Mto Msimbazi
eneo la Jangwani jana, alipokwenda kuangalia athari za mafuriko
walizopata wananchi yaliyotokana na mvua inayoendelea kunyesha jijini
Dar es Salaam.
Rais Kikwete jana alionekana kukerwa waziwazi na kitendo cha polisi kuwazonga
na kuwasukuma wananchi waliokusanyika eneo la Jangwani kumsikiliza.
Tukio hilo lilitokea alipotembelea maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Baada ya kufika eneo hilo saa tisa alasiri, polisi
waliokuwa wakiimarisha ulinzi walianza kuwasukuma wananchi hasa kule
walipokuwa wakielekea alikokuwa Rais Kikwete.
Mara kadhaa, Rais Kikwete alisikika akiwataka polisi kuacha kuwabugudhi badala yake wasogee upande wake.
Kutokana na askari hao kutotii amri yake,
alimwagiza Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman
Kova aliyekuwapo kuwakataza askari hao.
“Jamani, waacheni waje kwa nini mnawapiga? Mbona
hamsikii? Kova hebu waambie askari wako wawaache kuwasumbua,” alisikika
Rais Kikwete akisema huku akionyesha mkono kwa ishara ya kuwaita
wananchi wasogee upande wake.
Baada ya agizo hilo, Kamanda Kova aliwazuia askari kuwasukuma wananchi na ndipo walipoacha.
Akiwahutubia, Rais Kikwete alimwagiza Mhandisi wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Eliseus Mtenga kuchukua hatua za haraka
kushughulikia changamoto ya kuziba kwa Daraja la Jangwani ili kudhibiti
mafuriko yanayoendelea kuathiri wakazi wa eneo hilo.
Alisema hakuna sababu ya kuagiza Jeshi la Ulinzi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kushughulikia changamoto hiyo kwa kuwa
ni kazi ndogo inayoweza kutafutiwa ufumbuzi kwa muda mfupi.
“Huu uchafu ni wa kuondoa haraka, hakuna sababu ya
kuleta wanajeshi hapa. Mvua hizi bado zinanyesha, tusisubiri hali
iendelee kuwa mbaya,” alisema Rais Kikwete.
Mhandisi Mtenga aliahidi kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo haraka.
Katika hatua nyingine; mvua zinazoendelea kunyesha
zimesababisha Shule ya Msingi Msasani kujaa maji, kuvunjika madaraja na
kupanda kwa gharama za bidhaa ikiwamo chakula.
Goba
CHANZO: MWANACHI
Shule hiyo imejaa maji katika vyumba vinane huku waathirika
wakuu wakiwa ni wanafunzi wa darasa la saba, chekechea na wenye ulemavu
wa kutosikia.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Egidius Mujunangoma
alisema wanafunzi wa darasa la saba walikuwa wakijiandaa kwa mitihani ya
Moko ya Mkoa wa Dar es Salaam inayotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.
Alisema hata ofisi yake pia imejaa maji pamoja na
maktaba ambako vitabu vyote vimeharibika... “Sina mahali pa kukaa,
katika ofisi yangu sijafanikiwa kutoa kitu.”
Alisema licha ya kuwapo maji hayo, wanafunzi
wanaendelea na masomo wakitumia madarasa yaliyobaki ambayo hutumiwa na
wanafunzi wote.
Mujunangoma alisema afya za wanafunzi zipo
hatarini kutokana na maji hayo kutoa harufu mbaya na kwamba chemba
nyingi za eneo hilo zimefunguliwa.
Goba
Shule za sekondari Mbopo na Njechele, nazo
zimefungwa kutokana na mvua hizo kukata mawasiliano kati ya eneo la Goba
na Madale baada ya daraja kubomoka.
Mwanafunzi wa Mbopo, Sadick Khalfani alisema wamefunga shule kutokana na kuvunjika kwa daraja hilo.
“Shule imefungwa, tutapita wapi? Wa Goba hawawezi
kwenda Madale na sisi wa huku hatuwezi kuvuka, maji ni mengi, ” alisema
Khalfani.
Wakazi wanaoishi eneo la Madale wamelalamikia maisha kupanda kutokana na kuvunjika daraja hilo.
Walisema wanalazimika kununua kilo moja ya unga wa sembe kati ya Sh1,500 hadi 2,000. Mmoja wa wakazi hao, Waitara Matiku alisema wanapata wakati mgumu kutokana na kupanda kwa gharama za maisha huku wakiwa hawafahamu lini watapata nafuu hata ya kuwekewa daraja la muda.
Walisema wanalazimika kununua kilo moja ya unga wa sembe kati ya Sh1,500 hadi 2,000. Mmoja wa wakazi hao, Waitara Matiku alisema wanapata wakati mgumu kutokana na kupanda kwa gharama za maisha huku wakiwa hawafahamu lini watapata nafuu hata ya kuwekewa daraja la muda.
Mkazi mwingine, Mariamu Mrope anayejishughulisha na uchuuzi wa
mboga alisema biashara imekuwa ngumu kwa kuwa wateja wake wakuu walikuwa
wanatoka upande wa pili wa Madale. Alisema wanalazimika kukodi pikipiki kwa Sh7,000
hadi 10,000 kutegemea na hali iliyopo. Kama mvua inanyesha nauli huzidi,
wakifika kwenye maji hulazimika kukodi tena vijana ambao huvusha mizigo
yao.
CHANZO: MWANACHI
No comments:
Post a Comment