Bernard Kamilius Membe alianza elimu ya msingi mwaka 1962 katika Shule ya Rondo - Chiponda na alihitimu mwaka 1968, baadaye alikwenda kuendelea na masomo ya sekondari katika Seminari ya Namupa na kusoma kidato cha kwanza na nne kati ya mwaka 1969-1972. Alisoma kidato cha tano na sita katika Seminari ya Itaga mkoani Tabora kuanzia mwaka 1973 hadi 1974.
Historia yake
Benard Membe alizaliwa Novemba 9, 1953 katika
Kijiji cha Rondo-Chiponda, Wilaya ya Lindi hivyo atatimiza miaka 62,
Novemba mwaka huu. Ni mtoto wa pili kati ya saba wa familia ya Mzee
Kamillius Anton Ntanchile na mama Cecilia John Membe. Hivi sasa ni
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa.
Membe alianza elimu ya msingi mwaka 1962 katika
Shule ya Rondo - Chiponda na alihitimu mwaka 1968, baadaye alikwenda
kuendelea na masomo ya sekondari katika Seminari ya Namupa na kusoma
kidato cha kwanza na nne kati ya mwaka 1969-1972. Alisoma kidato cha
tano na sita katika Seminari ya Itaga mkoani Tabora kuanzia mwaka 1973
hadi 1974.
Maandiko kadhaa yanaonyesha kuwa Membe aliwahi
kusomea upadri kwa miezi kadhaa kabla hajajiunga na Seminari ya Itaga
akiwa mmoja kati ya vijana 11 walioshawishiwa na alichaguliwa kujiunga
na Seminari Kuu ya Peramiho, Songea.
Ndoto ya Membe kusomea upadri huko Peramiho
ilianza kuyumba polepole baada ya matokeo ya kidato cha nne kutoka
yakionyesha kuwa amefaulu vizuri. Hali hiyo ilimfanya Askofu Mkuu wa
Jimbo la Mtwara wakati huo, Maurus Libaba (marehemu), amshawishi ahamie
Itaga Seminari kusoma kidato cha tano na sita.
Membe alijiunga na JKT, kwa mujibu wa sheria.
Baadaye alifanya kazi serikalini miaka miwili ili kutekeleza Azimio la
Musoma ambalo lilitaka watu wote waliomaliza kidato cha sita kufanya
kazi miaka miwili kabla ya kujiunga na masomo ya chuo kikuu.
Baada ya kumaliza JKT, Membe hakukumbuka tena
upadri, badala yake aliajiriwa kwenye Ofisi ya Rais na kufanya kazi kwa
miaka sita ndipo alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kusomea Shahada
ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma kuanzia mwaka 1980 hadi
alipohitimu mwaka 1984.
Japokuwa ufaulu wake ulikuwa wa daraja la kwanza,
alikataa “ofa” ya kuendelea na jahazi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam la
kuwa mhadhiri msaidizi kwa sababu Ikulu ilimtaka arejee kazini mara
baada ya masomo. Moja ya majukumu aliyoisaidia Ikulu ni pamoja na kuchambua masuala ya Usalama wa Taifa na aliifanya kazi hiyo kwa mafanikio.
Membe alijiendeleza kitaaluma kwa kujiunga na Chuo
Kikuu cha Johns Hopkins, Marekani mwaka 1990 akisomea Shahada ya
Uzamili (MA) ya Uhusiano wa Kimataifa na kuhitimu mwaka 1992.
Baada ya kuhitimu pamoja na kuisaidia Ikulu
kipindi kirefu, Membe alihamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje mahali
alipokaa kwa miaka tisa (1992–2000) akishughulika na kazi ngumu ya
kuwashauri mabalozi, kabla ya kuamua kujiunga katika siasa za moja kwa
moja.
Membe ni mume wa Dorcas Masanche tangu mwaka 1986 na wamefanikiwa kuwa na watoto watatu, mmoja ni wa kike na wawili ni wa kiume.
Mbio za ubunge
Mbio za ubunge
Safari yake kisiasa ilianza mwaka 2000 kwenye
Uchaguzi Mkuu alipoomba ridhaa ya ubunge Jimbo la Mtama mkoani Lindi kwa
tiketi ya CCM. Uchaguzi ulipofanyika, CCM ikaibuka na ushindi ikiviacha
vyama vingine kwa mbali. Membe akachaguliwa na wananchi wa Mtama wakati
huo akiwa na miaka 47.
Mwaka 2005, CCM ilimrejesha kutafuta ushindi wa
Mtama kwa mara ya pili na bahati yake ikawa nzuri kwa sababu Isack
Wolfgans Ndaka wa TLP na Said Hamis Mtepa wa CUF hawakumpa upinzani
mkubwa hivyo alitetea ubunge wake kwa kupata asilimia 79.3 ya kura.
Rais Jakaya Kikwete alimteua kuwa Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani kuanzia Januari 2006 hadi Oktoba 2006 alipomhamishia
Wizara ya Nishati na Madini Oktoba 2006 ambako alishikilia wadhifa wa
unaibu waziri kwa mwaka mmoja hadi Novemba 2007.
Desemba 2007, Membe alipanda ngazi na kuwa Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akichukua nafasi ya Dk
Asha-Rose Migiro na alidumu katika wizara hiyo hadi awamu ya kwanza ya
JK ya miaka mitano ilipokamilika.
Membe aliendelea kuomba ridhaa mwaka 2010, ambao
ulikuwa mwepesi zaidi. Aliongeza ushindi kutoka asilimia 79.3 za mwaka
2005 hadi asilimia 81.76 mwaka 2010 kwenye Jimbo la Mtama.
Baada ya kuwa mbunge kwa kipindi cha tatu, Rais
Kikwete alimteua tena kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, nafasi ambayo ameendelea kuwa nayo hadi sasa.
Mbio za urais
Miaka 15 ya Membe kuwatumikia wana Mtama imekoma
baada ya yeye mwenyewe kutangaza rasmi kuwa hatakuwamo kwenye msafara wa
wasaka ubunge jimboni humo Oktoba mwaka huu. Kuaga huko kumetafsiriwa
kwamba anakwenda kuisaka ofisi ya juu zaidi, Magogoni.
Wakati anawaaga wana Mtama tayari kumekuwa na
ushahidi kuwa amekuwa akijipanga kwa ajili ya azma hiyo muda mrefu
uliopita na si vibaya kusema yeye ni kati ya wasaka urais kupitia CCM
ambao wamefanya maandalizi ya muda mrefu.
Nguvu yake
Membe ni mwanadiplomasia aliyebobea na ana nguvu
inayodhihirika kimataifa. Amekuwa katika Wizara ya Mambo ya Nje akiwa
mtumishi wa kawaida, kwa miaka minane na baadaye waziri wa wizara hiyo
hiyo kwa takriban miaka mingine minane.
Udhaifu wake
Uzoefu huo wa miaka 16 kwa ujumla umemrusha hadi kuchaguliwa
kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri wa Nchi za Jumuiya ya Madola
(CMAG) Novemba 2013 huko Sri Lanka. Kabla ya hapo, wadhifa huu, mara
nyingi, ulikuwa ukishikiliwa na viongozi kutoka nje ya bara la Afrika.
Nguvu ya pili ya Membe iko katika uzoefu wake
kwenye masuala ya utendaji ndani ya serikali na usalama wa nchi. Kwa
kifupi Membe ni kachero mzoefu na ameifanya kazi hiyo tangu alipomaliza
kidato cha sita na ilifika wakati akawa hadi msaidizi wa mkuu wa Idara
ya Usalama wa Taifa. Kwa hiyo, anaijua nchi hii vizuri na ana taarifa za
kutosha za mambo mengi nyeti yaliyojiri tangu enzi hizo.
Kingine kinachompa nguvu ni uungwaji mkono ndani
ya CCM. Huyu jamaa anaungwa mkono na kundi kubwa ndani ya CCM na naweza
kusema anavutana na makada wawili hivi, kati ya wasaka urais. Amekuwa
akigombea na kushinda nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM tangu
mwaka 2007 na tena akachaguliwa mara ya pili mwaka 2012 kwenye Mkutano
Mkuu wa Nane wa CCM (akishinda kupitia kundi la kifo) kwa kupata kura
1,451 nyuma ya Stephen Wasira, Mwigulu Nchemba na January Makamba tena
kukiwa na shinikizo kubwa kutoka kwa mahasimu wake kisiasa.
Membe ana nguvu isiyoweza kubezwa katika misimamo
kwenye masuala ya msingi. Mfano, amekuwa akitetea waziwazi suala la
uraia pacha bila kujali kuwa chama chake kimekuwa hakilitaki suala hilo
tangu enzi za Mwalimu Nyerere.
Pia Membe amekuwa akisimama kidete kumtetea Rais
Robert Mugabe wa Zimbabwe wakati mataifa ya Magharibi yakiwa yamemtenga
na kutomtambua bila kusahau kupinga sera za Magharibi dhidi ya Palestina
(misimamo mingine ni ya nchi na amekuwa akiisimamia ipasavyo).
Membe ana nguvu nyingine kimataifa kwa maana ya kukubalika na kupanga mipango inayoweza kuleta tija na kulinufaisha Taifa.
Ni katika uongozi wake wa Wizara ya Mambo ya Nje,
ndipo Serikali ya Tanzania ilipofanikiwa kuwakaribisha viongozi wa dola
zinazoongoza dunia; Rais Xi Jinping wa China na Barack Obama wa Marekani
tena kwa mapokezi ya kiwango cha juu.
Udhaifu wake
Moja ya udhaifu wa Membe ni upole uliozidi. Ni
mpole sana; mpole kupita kiasi. Watu wa karibu yake wanasema kwamba kuna
wakati anakuwa na huruma hata katika masuala yanayohitaji avae ngozi ya
simba.
Kwa hali ya nchi yetu ilipofikia, Taifa linahitaji
rais mkali kidogo na ikiwa ataendeleza upole wake huo utakuwa udhaifu
mkubwa mno kumkabidhi dola.
Udhaifu mwingine wa Membe ni kushindwa kuelewana
na maadui wake kisiasa. Wakati Rais Kikwete anaisaka Ikulu, ni Membe na
washirika wengine waliosimama kidete na kufanya kazi pamoja hadi
akashinda.
Miaka michache baadaye aliokuwa nao kundi moja
wakageuka kuwa maadui wa kutupwa na kila mmoja ameshindwa kurudi chini
na kuondoa “uhasama” uliopo. Huu ni udhaifu kwa kiongozi na
mwanadiplomasia wa kimataifa.
Taswira nyingine ya udhaifu wa Membe ni utata. Membe ni kati ya viongozi watata.
Mei 2014, akiwa bungeni Dodoma aliutangazia umma
na hata kunukuliwa na vyombo vya habari vya kimataifa akiishutumu Rwanda
kwamba inawafadhili waasi wa kikundi cha M23 kinachosumbua Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) na alidai kuwa M23 ni raia wa Rwanda.
Matamshi hayo yalikuwa hatari na tata kuwahi kutamkwa na mwanadipolomasia wa ngazi ya kimataifa kama Membe. Katika suala la rada, pia Membe alituonyesha utata
mkubwa. Mei 2011, alikataa uamuzi wa Kampuni ya BAE kuilipa Tanzania
Dola za Marekani 29.5 milioni kupitia mfumo wa “msaada” (sadaka) akisema
msaada hauwezi kuruhusiwa kama malipo hayo yatafanyika, akasisitiza
kuwa “watu hawa wamechanganyikiwa na wanajaribu kujitoa kwenye kashfa
hii na kusukuma mzigo kwa serikali ili dunia iamini kwamba Tanzania ni
nchi ya kifisadi na haiaminiki”.
Pamoja na kauli hiyo ya kuwashughulikia BAE, Membe
hakuwahi kuwalaumu wala kuwashutumu wale wote waliohusika na rushwa
katika kashfa hiyo.
Hata Mei 2012, Mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward
Hoseah alipotamka kwamba hakuna Mtanzania aliyehusika kwenye kashfa ya
ununuzi wa rada na hata habari hizo ziliporipotiwa na Gazeti la ‘Daily
News’ la Machi 31 mwaka huo, bado Membe hakujitokeza hadharani akiwa
Waziri wa Mambo ya Nje kupinga kauli hiyo au kutoa maoni yake juu ya
wizi huo. Unaweza kujiuliza, nini ulikuwa uwajibikaji wa Membe katika
jambo kubwa kama hili?
Nini kinaweza kumfanya apitishwe?
Jambo moja kubwa linamlofanya Membe atazamwe kama
mmoja wa watu wanaoweza kuvuka kigingi cha CCM na hatimaye kuteuliwa
kuwa mteule wa urais ndani ya CCM ni ukaribu wake na Rais Kikwete.
Mpaka sasa hakuna anayeweza kuthibitisha kama
Kikwete anampigia chapuo Membe, lakini kama taarifa hizo ni kweli, basi
zitamrahisishia njia.
Kingine kinachoweza kumvusha Membe ni kutoandamwa
na kashfa. Hata alipokuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini huku kashfa
ya Richmond ikinguruma, Membe hakuhusishwa hata kidogo na hadi sasa
ameendelea kuwa mmoja wa viongozi ambao hawatajwi katika kashfa mbaya za
rushwa. Taswira hii iliyojijenga kwamba yeye anaweza kuwa miongoni mwa
viongozi wasiopenda ufisadi na wanaokataa kujihusisha nao, inaweza
kumfanya aonekane kuwa chaguo la CCM.
Kitu kingine kinachoweza kumbeba ni kusimamia
ukweli. Membe ana rekodi ya kusimamia ukweli hata kama utamuumiza na
kuna nyakati anafanya hivyo bila kujali hatari zinazoweza kumkabili.
Mathalani, mwaka 2001/2002 aliposimama kishujaa
dhidi ya aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utawala Bora, Dk Hassy
Kitine kuhusu kashfa ya kutumia fedha za serikali kumtibu mke wake,
Saada Mkwawa nje ya nchi kwa kiwango cha Dola za Marekani 63,000.
Asipopitishwa (Mpango B)
Hitimisho
CHANZO: MWANANCHI
Pamoja na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), chini ya
Kaimu Mwenyekiti Richard Ndasa kuandika barua Wizara ya Afya ili
kumsafisha Kitine na mkewe, Membe alisimama kwa miguu yote na kuonyesha
ubadhirifu huo kwa uwazi hadi Bunge likachukua hatua za kinidhamu dhidi
ya Kitine na genge lake.
Nini kinaweza kumwangusha?
Kama kuna jambo lililo wazi linaloweza kumwangusha Membe katika safari yake ya kuitafuta Ikulu ni makundi. Kiongozi huyu amekwishajijengea kundi kubwa ndani ya CCM kwa kipindi kirefu ambalo linapambana na makundi hasimu.
Ikiwa CCM itahitaji kuwa na mgombea ambaye hana makundi na atakiunganisha chama, Membe anaweza kuwekwa pembeni. Kitu kingine kinachoweza kumtupa Membe ni misimamo
yake katika baadhi ya mambo ambayo kuna nyakati yamekwenda hata kinyume
na mtazamo wa chama chake.
Kuna wakati Membe huthubutu kufanya mambo ambayo
wenzake hawayapendi hasa katika nyanja za kimataifa. Ikiwa CCM itahitaji
Rais anayesikiliza zaidi sauti za chama chake, Membe anaweza kuwa nje.
Asipopitishwa (Mpango B)
Membe asipopitishwa na chama chake nadhani
atawekeza nguvu kwenye shughuli za kidiplomasia kwa maana ya diplomasia
ya kimataifa na kusaidia jumuiya ya kimataifa katika utatuzi wa migogoro
mbalimbali kutokana na uzoefu alio nao.
Lakini pia anaweza kutumia ujuzi na uzoefu wake
kufanya shughuli za ujenzi wa chama chake katika ngazi za juu kwa sababu
watu wa aina yake ni “tunu” muhimu.
Na mwisho anaweza kutumika katika kushauri masuala
ya ulinzi wa nchi yetu ukizingatia kwamba amekuwa kwenye Idara ya
Usalama wa Taifa kwa kipindi kirefu.
Hitimisho
Membe ni mmoja wa wanasiasa wenye ndoto za juu mno hapa
Tanzania. Ndoto zake hizo zinasababisha kambi nyingine zinazosaka urais
ndani ya CCM zisilale usingizi.
Ana ufuasi mkubwa miongoni mwa wana CCM na ni mtu
mashuhuri kwamba akikabidhiwa nafasi ya uteule ndani ya CCM, hakuna
atakayeshtuka. Nadhani alianza harakati za urais kipindi kirefu na
amekwishajipanga vya kutosha. Yeye ni miongoni mwa wana CCM wachache wenye
uwezekano wa kupenya lile “chekecheo kuu”. Namtakia kila la heri katika
safari yake hiyo.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment