Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Anna
Mgwira amesema chama hicho hakina matatizo na Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) na hata sasa kinasubiri majibu ya barua yao waliyoituma
kwa umoja huo kuomba kuunganishwa.
Alisema ACT-Wazalendo wanaunga mkono muungano wowote wa vyama vya upinzani nchini ulio halali. “Hatuna matatizo na Ukawa tunaunga mkono muungano wowote wa upinzani ulio halali,” alisema kiongozi huyo
Alisema tangu waandike barua ya kuomba mwongozo wa namna ya kujiunga na Ukawa, bado hawajapata mrejesho. “Tunatamani kuunganisha nguvu katika siasa za
vyama vya upinzani na sasa tunasubiri majibu ya barua yetu ya kuomba
kuingia Ukawa,” alisema.
Alisema kuwa chama hicho kimepokewa vizuri na
wananchi wa mikoa mbalimbali nchini na katika ziara ya awamu ya kwanza
walifanikiwa kuingiza jumla ya wanachama wapya 700. “Tumepokewa vizuri mikoani tumefanikiwa kuingiza
wanachama wapya na hoja ya umoja na uzalendo watu wameipokea vizuri,”
alisisitiza Mgwira.
Akipokea misaada katika hospitali hiyo Muuguzi
Mfawidhi, Sifael Masawe alisema kwamba misaada hiyo itasaidia kupunguza
shida za wagonjwa waliofika hospitalini hapo na kuwataka wengine kujitokeza kuwaunga mkono.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment