Kamanda wa polisi wa mkoani Morogoro, Leonard Paul
Wakati msikiti wa Sunni uliopo Kidatu
wilayani Kilombero ukimkana Hamadi Makwendo aliiyeuawa katika tukio la
kuwakamata watu 10 wanaotuhumiwa kuhusika na vitendo vya ugaidi, dereva
wa bajaji iliyowabeba baadhi ya watuhumiwa hao, amemuelezea mtu huyo
kuwa alikuwa hana shughuli za kikazi zaidi ya kucheza karate.
Polisi aliyejeruhiwa kwenye sakata hilo na ambaye amehamishiwa kwenye hospitali ya polisi mjini Morogoro, pia amesimulia mkasa uliosababisha ajeruhiwe huku kukiwa na taarifa kuwa watuhumiwa hao 10 wamehamishiwa jijini Dar es Salaam kwa mahojiano zaidi.
Polisi aliyejeruhiwa kwenye sakata hilo na ambaye amehamishiwa kwenye hospitali ya polisi mjini Morogoro, pia amesimulia mkasa uliosababisha ajeruhiwe huku kukiwa na taarifa kuwa watuhumiwa hao 10 wamehamishiwa jijini Dar es Salaam kwa mahojiano zaidi.
Watu hao walimakatwa mapema juzi usiku kwenye
msikiti wa Sunni uliopo Kidatu baada ya wasamaria wema kulitaarifu Jeshi
la Polisi kuhusu kuwapo kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya
uhalifu.
Habari za uhakika zilizopatikana ndani ya Jeshi la
Polisi zinasema watuhumiwa hao wamehamishiwa jijini Dar es Salaam kwa
ajili ya mahojiano zaidi.
Kamanda wa polisi wa mkoani hapa, Leonard Paul hakupatikana kuzungumzia suala hilo na hata alipotafutwa kwa
simu, mlinzi wake alipokea na kueleza kuwa bosi huyo wa polisi alikuwa
kwenye kikao kuanzia asubuhi na hakujua angemaliza wakati gani.
Mmoja wa viongozi wa msikiti wa Masjid Salah Al –
Fajih, Mohamed Manze alisema wao kama viongozi na waumini hawakuwa na
taarifa zozote za ujio wa watuhumiwa hao, na kwamba katika msikiti huo
wapo vijana wanne ambao huwa wanalala na kujisomea.
Alisema siku ya tukio watuhumiwa hao walifika
msikitini hapo saa 4:00 usiku wakati ibada ya mwisho ikiwa imeshafanyika
na waumini kutawanyika. Alisema walitumia mwanya huo kuingia na
kujihifadhi bila taarifa zozote kwa uongozi wa msikiti huo, jambo ambalo
ni kinyume na utaratibu za msikiti.
Hata hivyo, kiongozi huo alisema hawakupendezwa na
suala hilo na kwamba limewachafua na kuwaharibia sifa waumini na
msikiti wao. Alisema mtu aliyeuawa hakuwa muumini wa msikiti huo na
hafahamiki.
Alisema hawana nasaba na kikundi chochote
kinachojihusisha na uhalifu, na kulaani vikali watu wanaotumia dini hiyo
katika masuala aliyoyaita kuwa ya kihalifu.
Dereva wa bajaji asimulia
Dereva wa bajaji iliyobeba watuhumiwa hao katika
kijiji cha Kidatu wilayani Kilombero, Alphonce Maulusi amemwelezea Hamad
Makwendo, aliyeuawa kwenye tukio hilo kuwa ni mtu aliyekuwa
akijihusisha na mchezo wa kareti pamoja na masuala ya dini na hakuwa na
kazi maalumu.
Mwenyekiti wa kitongoji
Mulusi alisema hayo jana wakati akiongea na waandishi wa habari
waliotembelea kijijini hapo kwa lengo la kupata undani wa tukio
lililotokea juzi katika kijiji cha Chikago kata ya Kidatu wilayani
Kilombero ambapo watu 11 walikamatwa na polisi msikitini wakiwa na
vifaa mbalimbali vya milipuko pamoja na sare za jeshi.
Alisema siku ya tukio majira ya saa 3:00 usiku
akiwa katika eneo lake la kazi, walitokea watu 11 na kwamba watano kati
yao pamoja na mwenyeji ambaye ni marehemu walipanda katika bajaji yake ,
na wengine sita walipanda katika bajaji ya mwenzake.
Alisema watu hao wakiongozwa na mwenyeji wao
walitaka wapelekwe msikiti wa Sunni na kwamba wakati wote wa safari yao
mwenyeji wao ndiye alikuwa akizungumza lugha ya Kiswahili huku wenzake
wakisikiliza bila kujibu. “Tuliwafikisha hadi eneo walilotaka na kisha
tuligeuza na yule mwenyeji wao. Tulipofika Manyasini, tulisimamishwa na
polisi waliotaka kujua tumetoka wapi na tunaenda wapi. Yule mwenyeji
alishuka na kuanza kukimbia jambo lililofanya askari kuanza kumkimbiza
huku sisi tukifuatilia nyuma,” alisema.
Alisema mwenyeji huyo alipofika mbele kidogo
alimkata polisi mmoja na jambia na ndipo polisi walimpiga risasi na
baadaye kumchukua na kumpandisha katika gari lao.
Alisema wananchi walifika katika eneo hilo na
kuzingira gari hilo na kumshusha mtu huyo, huku wakitishia kuchoma moto
gari la polisi . Akizungumzia mwonekano wa watu hao, dereva huyo
alisema walivalia mavazi ya jamii ya kabila la Wahindi maarufu kama
Panjabi na umri wao ukionekana kati ya miaka 20 hadi 25 tofauti na
mwenyeji wao aliyeonekana mkubwa wa zaidi ya miaka 30.
Koplo Nasoro Dabi, ambaye alijeruhiwa katika tukio
hilo, alisema siku ya tukio, akiwa na askari wenzake walisimamisha
bajaji iliokuwa na abiria mmoja, Hamad Makwenda.
Alisema baada ya bajaji hiyo kusimama marehemu
alikimbia hali, iliyoashiria kuwa ni mhalifu na hivyo kuwalazimu askari
watatu, akiwamo yeye, kumkimbiza.
“Wakati tukimkimbiza, mimi nilikuwa mbele na
tulipofika katika eneo lenye giza, alichomoa jambia na kuanza
kunishambulia. Askari wenzangu waliokuwa nyuma yangu walifyatua risasi
na kupiga nyingine juu hali iliyosababisha wananchi wengi kujitokeza na
kuanza kumpiga kisha kumchoma moto,” alisema.
Alisema wakati tukio hilo likiendelea askari wengine walifanya mawasiliano na mkuu wa kituo cha Ruhembe na kuwaongezea nguvu.
Mwenyekiti wa kitongoji
Mweyekiti wa kitongoji cha Ikera, Mohamed Libaha
alisema siku ya tukio hilo alifuatwa na askari saa 8:00 usiku na
kutakiwa atoe malezo kama ana taarifa za wageni katika kitongoji chao.
Alisema bada ya kuwaambia kuwa hawana ugeni wowote, polisi waliwachukua watu hao pamoja na kiongozi wao wa dini, Ustadhi Maulid Sultani na kuondoka naye na hadi sasa hawana taarifa ya mintaarafu ya kiongozi huyo.
CHANZO: MWANANCHI
Alisema bada ya kuwaambia kuwa hawana ugeni wowote, polisi waliwachukua watu hao pamoja na kiongozi wao wa dini, Ustadhi Maulid Sultani na kuondoka naye na hadi sasa hawana taarifa ya mintaarafu ya kiongozi huyo.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment