Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amesema
serikali haitakimbia wala kuogopa ukuaji wa teknolojia nchini, bali
inajipanga kupambana na changamoto zinazojitokeza katika teknolojia hiyo
kwa kuwa inachangia katika ukuaji wa uchumi.Nchemba alisema hayo wakati akizindua huduma ya kifedha kwa njia ya
mtandao ambayo imeshirikisha Benki ya NMB na Kampuni ya simu za mkononi
ya Airtel, itakayowawezesha wateja wake kutuma au kutoa fedha kutoka
kwenye akaunti ya NMB kwenda kwenye akaunti zao za Airtel money kupitia
simu za mkononi.
Alisema hakuna haja ya kupingana na ukuaji wa teknolojia isipokuwa
kinachotakiwa ni kujiandaa kwenda sambamba na ukuaji huo kwa kujipanga
ya kupambana na baadhi ya changamoto zinazojitokeza kwa kuwa inachangia
kwa kiwango kikubwa ukuaji wa uchumi nchini.
Akitolea mfano suala la huduma za kifedha, Nchemba alisema mpaka sasa
umesaidia wananchi wa mijini na vijijini kupata huduma hiyo kwa urahisi
zaidi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment