Profesa Sopheter Muhongo
Umoja wa Watu wenye
Ulemavu katika Mkoa wa Mwanza unaojulikana kwa jina la ‘Walemavu
tunaweza’, umesema nchi inapaswa kuongozwa na mtu mwenye uelewa wa
masuala ya gesi ili atumie nishati hiyo, kuwaletea wananchi maendeleo.
Umoja huo umeenda mbali zaidi na kumtaka aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo agombee nafasi hiyo kwa kuwa ana uwezo, hekima na utalaamu wa kutosha kuhusu masuala ya gesi na kuongoza nchi.
Umoja huo umeenda mbali zaidi na kumtaka aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo agombee nafasi hiyo kwa kuwa ana uwezo, hekima na utalaamu wa kutosha kuhusu masuala ya gesi na kuongoza nchi.
Mwenyekiti wa bodi ya umoja huo, Makubi Makubi
alisema wamekaa chini na kutafakari kwa muda mrefu na kubaini kwamba
Muhongo anaweza kuwa chaguo sahihi kwa Watanzania, kwani anaweza kutumia
utaalamu wake wa gesi kuibadilisha nchi na kuifanya iwe na maendeleo
endelevu
“Sisi watu wenye ulemavu Mwanza, kupitia umoja
wetu, tumekaa kwa muda mrefu na kutafakari kwamba nani anaweza kugombea
urais katika uchaguzi mkuu ujao. Tukaona mtu sahihi ambaye anaweza
kuwaletea maendeleo Watanzania ni Muhongo, kwani katika utendaji wake wa
kazi ana maamuzi sahihi,” alisema Makubi.
Mwenyekiti wa umoja huo, Veronica Mtiro alisema
kuwa Muhongo ni mtaalamu wa gesi na kwamba kutokana na utaalamu wake
anaweza kuchochea maendeleo ya taifa.
Hii ni mara ya pili wakazi wa Mwanza kumtaka
Profesa Muhongo agombee urais. Hivi karibuni Wazee wa Mkoa huu nao
walijitokeza kuzungumza na waandishi wa habari na kumtaka Muhongo
achukue fomu ya kuwania nafasi hiyo ndani ya CCM.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment