
Moja ya visima vinavyotumiwa na wanawake kuteka maji.
Maadhimisho ya ‘Wiki ya Maji’, ambayo hufanyika
Machi 16 hadi Machi 22 kila mwaka yalianza jana nchini kote. Mwaka huu
maadhimisho hayo yanafanyika kitaifa mkoani Mara na Serikali imesema
kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Maji kwa Maendeleo Endelevu’.
Pamoja na maadhimisho hayo kufanyika kitaifa katika moja ya mikoa nchini, wilaya na mikoa mingine pia huadhimisha ‘Wiki ya Maji’, lengo likiwa ni kujadili kero na changamoto za upatikanaji wa huduma ya maji nchini, ambapo Serikali huelezea utekelezaji wa sera na mipango ya maendeleo katika Sekta ya Maji.
Pamoja na maadhimisho hayo kufanyika kitaifa katika moja ya mikoa nchini, wilaya na mikoa mingine pia huadhimisha ‘Wiki ya Maji’, lengo likiwa ni kujadili kero na changamoto za upatikanaji wa huduma ya maji nchini, ambapo Serikali huelezea utekelezaji wa sera na mipango ya maendeleo katika Sekta ya Maji.
Sherehe za maadhimisho hayo zilianza mwaka 1988.
Pamoja na maadhimisho hayo kutumia fedha nyingi kila mwaka na viongozi
kutoa ahadi lukuki ambazo wananchi wengi hawaoni kama zinatekelezeka,
uhaba wa maji umeendelea kuwa kero kubwa mijini na vijijini.
Kama ilivyokuwa wakati wa maadhimisho hayo miaka
iliyopita, maadhimisho ya mwaka huu tayari yameshuhudia wananchi
wakiuliza maswali magumu kuhusu hali mbaya ya maji nchini. Katika toleo la gazeti hili jana, wananchi
waliohojiwa kuhusu maadhimisho ya ‘Wiki ya Maji” walisema maadhimisho
hayo hayana faida yoyote na kuendelea kuwapo ni matumizi mabaya ya fedha
za walipakodi.
Hoja ya wananchi wengi ni kwamba Serikali bado haijui ukubwa wa tatizo la maji nchini. Kwamba haijatambua kwamba tatizo hilo linachangiwa
sana na ongezeko la idadi ya watu, ukuaji wa shughuli za uzalishaji
viwandani, umwagiliaji, uchimbaji madini, ufugaji na sekta nyingine.
Wanasema Serikali inaonekana kujikita zaidi katika
ukusanyaji wa takwimu nyingi zisizo na uhalisia kuhusu tatizo la maji,
pasipo kutafsiri takwimu hizo katika muktadha wa uharibifu wa vyanzo vya
maji, ubovu wa miundombinu ya kusambaza maji, mipango mibovu ya
kushughulikia tatizo la maji, athari za vitendo vya rushwa na ufisadi
katika kuendesha na kusimamia miradi ya maji.
Inashangaza kuona kuwa, tatizo la maji vijijini na
mijini limezidi kuwa kubwa, licha ya kuwapo mikakati mbalimbali ya
kulitatua. Hii ni pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2015; Mpango wa
Maendeleo wa Milenia 2015; Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza
Umaskini Tanzania; na Programu ya Maendeleo ya Kisekta iliyoanza mwaka
2007/08.
Lakini pia inashangaza kuona Serikali ikishindwa
kuweka mifumo ya usimamizi wa miradi ya maji, hivyo kuwapo baadhi ya
watumishi wake wanaohujumu miradi hiyo, ikiwamo iliyoanzishwa na Benki
ya Dunia (WB). Kutokana na hujuma hizo, benki hiyo miaka miwili
iliyopita iliamua kusimamia yenyewe udhibiti wa matumizi mabaya ya fedha
inazotoa kwa miradi hiyo, lakini tatizo hilo bado halijaisha hadi leo.
Tatizo hapa ni mfumo wa ufisadi uliojikita
serikalini, hivyo kuchangia kufanya ahadi za Serikali za upatikanaji wa
maji kutotekelezwa.
CHANZO: MWANANCHI
Kwa muda mrefu sasa, limekuwapo pendekezo linaloitaka Serikali
kuunda chombo kinachoitwa Wakala wa Maji, kama ilivyo kwa Wakala wa
Barabara, yaani Tanroads. Haijulikani kwa nini Serikali haitekelezi
pendekezo hilo, hasa tukiangalia mafanikio na ufanisi ambao Tanroads
imeupata katika muda mfupi tangu ianzishwe. Tunadhani wakati umefika kwa
Serikali kuona upatikanaji wa maji kama haki ya msingi kwa wananchi. Ikumbukwe kwamba suala la upatikanaji wa maji ni
sehemu ya makubaliano ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia kupitia
Mpango wa Malengo ya Milenia unaoratibiwa na Umoja wa Mataifa (UN).
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment