
Mama na mwana
Mvua baridi na jua, nguo ulinifunika, Nilipoanza kulia, na nyimbo zilikutoka, Mema ulonipatia, jamii yanufaika, Mama nakupenda sana, mama hakuna mwingine.
Zawadi gani nikupe, mama uliyenizaa,
Moyo ukae mweupe, furaha ikakujaa,
Deni wapi nikalipe, ni zamu ya kukulea,
Tuseme basi Amina, iwe heshima kwa mama.
Ulilala kwa kilepe, pale nilipougua
Ulisaka kama kupe, mwanao nisife njaa,
Nikisema nikulipe nitamaliza dunia,
Tuseme basi Amina, iwe heshima kwa mama.
Mvua baridi na jua, nguo ulinifunika,
Nilipoanza kulia, na nyimbo zilikutoka,
Mema ulonipatia, jamii yanufaika,
Mama nakupenda sana, mama hakuna mwingine.
Nakupenda sana mama, kweli hakuna mwingine,
Mama usishike tama, machozi yasinidone,
Na Mungu akupe mema, mabaya yasikuone,
Mama nakupenda sana, mama hakuna mwingine.
Usemi ningerudia, hivi nani kama mama
Elimu ulonipatia, hakuna dunia nzima,
Huzuni itanijia, tekelea ikihama,
Useme basi Amina, iwe heshima kwa mama.
CHANZO: MWANANCHI
Asante kwa yote mama, mwishoni najisemea,
Dua zako kwa labama, upate kuniombea,
Hakuna wa kukupima, Mlojo sijakosea
Mama nakupenda sana, mama hakuna mwingine.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment