
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahaman Kinana.
Chama cha Mapinduzi (CCM), kimesema
ubinafsishaji mashamba uliofanywa na Serikali miaka ya nyuma, haukuwa na
tija kwa wananchi hata kwa wakati huo.
Vilevile, CCM imedai kuwa uwekezaji huo ulilenga zaidi kuwapa haki matajiri wachache na kuwanyima maskini, jambo ambalo limesababisha kuwapo migogoro mingi ya ardhi nchini. Kauli hiyo ilitolewa juzi na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa CCM, Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro.
Vilevile, CCM imedai kuwa uwekezaji huo ulilenga zaidi kuwapa haki matajiri wachache na kuwanyima maskini, jambo ambalo limesababisha kuwapo migogoro mingi ya ardhi nchini. Kauli hiyo ilitolewa juzi na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa CCM, Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro.
“Haikuwa sawa hata kidogo, maana ardhi
ilichukuliwa kwa watu tukaikabidhi kwa umma, hivyo baada ya kushindwa
kuiendeleza tulipaswa kuirudisha kwa wenye ardhi, siyo kuwapa watu
wengine ambao nao wameshindwa na hawataki kukiri kuwa wameshindwa...ni
aibu,” alisema Kinana.
Katibu huyo alisema kuwa uwekezezaji wenye tija ni
ule unaowanufaisha wananchi wote na siyo baadhi ya watu kama ilivyo
hivi sasa. Kinana alisema mpango huo ulitekelezwa bila ya
kuangalia masilahi ya wenye ardhi kwa siku za usoni, badala yake
uliangalia matajiri na kampuni kubwa pekee ambazo leo hii ndiyo chanzo
cha migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji.
Alisema kitendo cha wananchi kukodi ardhi na
kulipa fedha wakati ilikuwa mali yao, kinaamsha hasira na baadhi kuanza
kuichukia Serikali yao. “Hiyo ni sawa na kuendelea kukumbatia ukabaila
ambao hayati Mwalimu Juliusu Nyerere alishaufukuza na sisi tumekuwa
tukiupiga vita,” alisema.
Alitaja moja ya makosa ambayo Serikali inatakiwa
kuyajutia ni uuzwaji wa Kiwanda cha Bia (TBL), ambacho kwa maelezo yake
kilipanga kulima shayiri, lakini hadi sasa kimeshindwa na huwa kinaagiza
nje ya nchi wakati ardhi wanaikodishi kwa wananchi kwa gharama kubwa.
Mbunge wa Siha, Aggrey Mwanri, ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), alisema kuwa Ilani ya
Uchaguzi ya CCM imetekelezwa katika jimbo lake kwa zaidi ya asilimia
100.
Mwanri alisema katika jimbo lake, vijijini vyote vina maji safi na salama, umeme kila kijiji na barabara zinapitika wakati wote.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment