Mkutano wa usalama wa taifa unafanyika Elysée, siku moja tu baada ya
maandamano ya kihistoria mjini Paris na katika miji yote mengine ya
Ufaransa kupinga mashamblio ya kigaidi yaliyoitumbukiza msibani
Ufaransa.
Wakikabiliwa na kitisho kikubwa kabisa cha kutokea wimbi jengine la
mashambulio,rais wa Ufaransa Francois Hollande amekutana na waziri mkuu
Manuel Valls,waziri wa mambo ya ndani Bernard Caseneuve, na mwenzao wa
sheria Christiane Taubira pamoja na wakuu wa idara za usalama katika
kasri lake huko Elysée. "Ufaransa bado inakabiliwa na vitisho" alionya hapo awali rais Hollande
huku serikali yake ikiungama kumekuwa na "ufa" katika opereshini za
usalama zilizoanzishwa katika nyanja tofauti dhidi ya wafuasi wa itikadi
kali.
Wanajeshi 10 000 kusimamia usalama
Waziri mkuu Manuel Valls amesema kabla ya kuhudhuria mkutano wa
usalama katika kasri la rais kwamba jumla ya wanajeshi 10 000 watawekwa
katika kila pembe kuambatana na mpango madhubuti wa kupambana na
ugaidi-"Vigipirate"-Akizungumza na kituo cha televisheni cha BFMTV
waziri mkuu Manuel Valls amefafanua hatua za usalama zimeimarishwa
kuliko wakati wowote ule mwengine.Wanajeshi 5000 wanawekwa kulinda
masinagogi na shule za kiyahudi.Waziri mkuu Valls ameongeza kusema hata
misikiti italindwa kutokana na mashambulio yaliyotokea hivi karibuni
kufuatia mashambulio ya kigaidi yaliyoangamiza maisha ya watu
wasiopungua 17 wiki liyopita.
Jana umati wa watu, zaidi ya milioni tatu na nusu waliokuwa na nyuso za
huzuni na furaha waliteremka majiani mjini Paris na katika kila pembe ya
Ufaransa kuonyesha mshikamano na kulaani matumizi ya nguvu-maaandamano
yaliyofanyika wakati mmoja na yale ya viongozi zaidi ya 50 wa kimataifa
walioteremka pamoja na rais Francois Hollande hadi katika uwanjka
mashuhuri wa Place de la Republik mjini Paris. Zaidi ya watu milioni moja na nusu waliteremka mjini Paris kwa mujibu wa waziri wa mambo ya ndanmi Berard Caseneuve.
Maandamano hayo yalipangwa hapo awali kuwakumbuka wahanga wa mashambulio
ya kigaidi wakiwemo wachoraji wa jarida la tashtiti la Charlie Hebdo
waliouliwa jumatano iliyopita ,askari polisi mmoja wa tarafa aliyeuliwa
alkhamis na wayahudi wannme waliouliwa ijumaa katika duka la
kiyahudi-Casher ijumaa iliyopita.
Yalijipatia kipeo cha kimataifa na kutoa picha ya viongozi wa kimataifa
waliokamatana mikono,nyuso zimekunjwa hadi katika uwanja wa Place de la
Republique.Francois Hollande amezungukwa na kansela Angela
Merkel,kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas,waziri
mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu,,waziri mku wa Uengereza David
Cameon,mfalme wa Joradan,waziri mkuu wa Italy,tukiwataja kwa
uchache.
Mshikamano wa kimataifa dhidi ya ugaidi
Wakishangiriwa na umati wa watu walipowasili,viongozi hao wa
kimataifa walisalia kimya dakika moja kabla ya kurejea kataika kasri la
rais Elysée.Rais Hollande aliwaamkia familia za wahanga waliokuwa safu
ya mbele ya maandamano hayo. Hisia za mshikamano ndizo zilizojitokeza.Meya wa jiji la kaskazini la
Lille Martine Aubry anasema:"Nna furaha kuona umati mkubwa kama huu wa
watu kutoka asili,tamaduni ,na umri na mirengo tofauti ya kisiasa
waliosimama kidete kusema hatutaki ugaidi,.Kuwepo viongozi wa kimataifa
kunabainisha haya ni mapambano ya kimataifa." Wakati huo huo juhudi za kumsaka angalao mtuhumiwa mmoja anaesemekana
huenda amewasaidia waasisi wa tatu wa mashambulio ya wiki iliyopita
mjini Paris, zinaendelea.
CHANZO: DW KISWAHILI

No comments:
Post a Comment