
Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe
     
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali 
(PAC), imeiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuharakisha agizo la 
ukaguzi wa sekta ndogo ya sukari ili kupata ufumbuzi wa haraka.
Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe, akitoa maamuzi mara baada ya 
kuhojiana na TRA, alisema uingizwaji holela wa sukari una hatari kwa 
ukuaji wa viwanda vya ndani. “Tunataka taarifa ili tuweze kuwa na mikakati endelevu ya kuzuia 
sukari ya magendo, unasababaisha sukari inayozalishwa na viwanda vyetu 
na miwa ya wakulima ina kosa soko,” alibainisha.
Hivi karibuni, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, 
alipotembelea kiwanda cha sukari cha TPC mkoani Kilimanjaro, alielezwa 
jinsi sukari ya nje iliyojaa sokoni na wao kukosa pa kuiuza. Alisema watakutana na Wizara zinazohusika kujadili na kuanza 
operesheni maalum kwenye maduka mbalimbali na kukamatwa sukari ya nje na
 ya viwandani inayouzwa kwa wananchi kwa bei ndogo.
     CHANZO:
     NIPASHE
    
No comments:
Post a Comment