
“Kazi ya mafuta ya transfoma ni kupoza nguvu ya umeme mkubwa,” alisema
Injinia Kamuleka na kuongeza kuwa mafuta hayo pia huchanganywa na ya
gari.
Ile dhana ya kuwa mafuta ya
kupoza transfoma yanaibwa na wauza chipsi, imebainika siyo ya kweli
baada ya uchunguzi kuonyesha kuwa yanatumiwa viwandani kuendesha
mitambo, kuchanganywa katika vipodozi na mengine yakisafirishwa nchi za
nje.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa
wanaoiba mafuta hayo ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) pia huchukua
nyaya za shaba katika transfoma hizo kwa ajili ya kutengeneza mapambo
mbalimbali kama herini, mkufu na bangili. Kutokana na wizi huo, mwaka jana pekee transfoma
34 zenye ukubwa mbalimbali ziliibiwa mafuta na shaba, hivyo
kuisababishia Tanesco hasara ya Sh306 milioni.
Meneja Mwandamizi, Masoko na Mauzo wa Tanesco,
Injinia Nicholaus Kamuleka alisema utafiti uliofanywa na wahandisi wa
shirika hilo unaonyesha kuwa mafuta ya transfoma yanaibwa kwa ajili
shughuli mbalimbali.
“Kazi ya mafuta ya transfoma ni kupoza nguvu ya
umeme mkubwa,” alisema Injinia Kamuleka na kuongeza kuwa mafuta hayo pia
huchanganywa na ya gari.
Transfoma kubwa moja inaweza kuwa na lita 200 za mafuta wakati dogo kabisa lina ujazo wa lita 40. Kamuleka alisema pia hutumiwa na mafundi wa kienyeji kuchomelea vyuma ambao huyanunua kwa Sh5,000 kwa lita. Mmiliki wa kiwanda cha chuma kilichopo Mikocheni
ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema: “Sisi hatuwezi kuharibu
transfoma na kuchukua mafuta, sisi tunaletewa hapa hapa.”
Dhana ya chipsi
Injinia Kamuleka alikanusha kuwa mafuta ya
transfoma hutumiwa na wafanyabiashara kukaanga chipsi na kusema kuwa
harufu kali ya mafuta hayo isingefaa kwa matumizi ya kula.
Baadhi ya wafanyabiashara wa chipsi walisema ni vigumu kutumia mafuta hayo kwa kuwa yanauzwa bei ghali. “Huwezi kununua mafuta lita Sh10,000 kwa ajili ya biashara ya chipsi,
siyo kweli kabisa,” alisema mfanyabiashara wa Tabata, Elisha Mungai.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment