
Meja Generali Joseph Kapwani.
     
Sekta ya uchukuzi na usafirishaji imezidi kukua hususani anga kuongoza katika kuongeza uchumi wa taifa.
Hali hiyo inatokana na kuongezeka kwa mashirika zaidi ya 40 yaliyosajiliwa nchini kuratibu shughuli za usafiri wa anga. Hayo yamesemwa jana na Meja Generali Joseph Kapwani, Mkuu wa 
Kamandi ya Jeshi  la Anga aliyemwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na 
Usalama, aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekaji wa jiwe la 
msingi wa Hanga la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na maadhimisho 
ya miaka ya 40 ya chuo hiko.  
Jenerali Kapwani alisema kuanzishwa kwa jengo hilo ambalo litakuwa 
la kwanza nchini Tanzania kutoa  kozi ya uhandisi wa kutengeneza ndege 
na urubani ni jambo jema na hatua kubwa na muhimu ya kimaendeleo kwa 
taifa. Alisisitiza kuwa uanzishwaji wa kozi hiyo ya  utaongeza wataalamu 
na kuimarisha ufanisi wa kiutendaji sambamba na kukuza uchumi wa taifa 
kwani wadau wengi na watumiaji wa huduma za usafiri wa anga watanufaika. “Ili anga liwe salama linahitaji kuwepo na vyombo imara kama ndege 
ambazi ubora wake unategemea sana utaalamu wa wahandisi waliofunzwa 
vizuri na kuielewa vyema fani hiyo.” alisema Generali Kapwani.
Mkuu wa chuo hiko, Dk. Zacharia Mganilwa, alisema kuwa sekta ya 
anga ni nyeti katika uchumi wa nchi, ikisimamiwa vizuri kwa kuwa na 
wataalamu wenye weledi, inaweza ikaongeza kwa kiasi kikubwa pato la 
taifa. Aliongeza kuwa upande wa marubani wazawa kwa Tanzania idadi 
hairidhishi kutokana na takwimu zinazoonyesha kuwa mpaka  Juni, 2014 
Tanzania ilikuwa na marubani 533 na kati ya hao, 239 ni wazawa na 
waliobakia 294 ni wageni. 
CHANZO:
     NIPASHE
 

No comments:
Post a Comment