Social Icons

Pages

Saturday, January 03, 2015

PHIRI AWATAKA SIMBA KUTAFUTA CHANZO CHA KUFUNGWA

Aliyekuwa kocha wa Simba Mzambia Patrick Phiri amesema viongoi wa Simba wanatakiwa kutafuta chanzo cha kikosi cha timu hiyo kufanya vibaya katika michuano mbalimbali ligi kuu ya bara na si kukatisha mikataba ya makocha.
Phiri ameondoka nchini jana kuelekea kwao Zambia, baada ya Simba kukatisha mkataba wake wa kukinoa kikosi hicho kutokana na kwenda mwenendo wa kusua sua kwenye msimamo wa ligi. Akizungumza na NIPASHE kabla ya kuondoka na ndege ya Fast Jet jana asubuhi alisema Simba inapaswa kujua tatizo kubwa la ti u yao na si kubadilisha makocha kila kukicha.
"Viongozi wanapaswa kutafuta chanzo cha timu kufanya vibaya na si kukimbilia kukatisha mikataba ya makocha,"alisema Phiri. Alisema yeye kama kocha anaimani timu kufanya vibaya kunatokana na mambo mengi ikiwemo suala zima pia la mishahara ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa wachezaji kucheza chini ya kiwango wanapokuwa uwanjani.
Alifafanua zaidi ya kuwa Simba na timu nyingine wasipofanya hivyo watashindwa kukaa na makocha kwa muda mrefu kutokana na mwenendo mbaya utakaofanywa na timu zinazoshiriki ligi kuu ya bara iliosimama kwa muda ili kupisha Mapinduzi Cup.
Akizungumzia kwa upande wake alisema anawashukuru mashabiki wa Simba kwa kumkubali huku akiwataka kuendelea kuwa na moyo wa kuisapoti timu yao. Alisema pamoja na kuwa yeye ameondoka amewataka kumpa ushirikiano kocha mpya ambaye ameanza kibarua juzi huku akishuhudia kikosi hicho kikifungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika kombe la Mapinduzi.
Alisema ushirikiano watakautoa kwa kocha huyo utaisaidia timu hiyo kuweza kubadilika katika hatua ya tisa ya ligi kuu ya bara inayotarajia kuanza mara baada ya fainali ya kombe la Mapinduzi linaloendelea katika uwanja wa Aman Karume uliopo visiwani Zanzibar. Alisema ameondoka jijini baada ya viongozi wa Simba ambao walimuomba kuja kuinoa timu hiyo kuuvunja mkataba wake kutokana na kutoridhika na mwenendo mbovu wa timu hiyo. Simba inashika nafasi ya 10 katika msimao wa ligi kuu ya bara iliosimama kwa muda ili kupisha kombe la Mapinduzi, ikiwemo kuanza vibaya katika katika mapinduzi cup baada ya kufungwa na Mtibwa Sugar bao 1-0.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments: