Pages

Friday, January 23, 2015

MATUNDA YA BRN YAANZA KUONEKANA

Mtendaji Mkuu kutoka Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia utelezaji wa BRN kwa Tanzania Bara, Omari Issa.
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambao Serikali ya Tanzania imeanza kuutekeleza tangu Julai, 2013, umeleta matokeo makubwa ambayo yanaelezwa kuwa yatasaidia kukuza uchumi wa nchi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari baada ya semina liyohusisha viongozi mbalimbali visiwani Zanzibar juzi,  Mtendaji Mkuu kutoka Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia utelezaji wa BRN kwa Tanzania Bara, Omari Issa, mafanikio hayo yametokana na nidhamu ya utendaji kazi na mfumo uliowekwa na serikali.
Katika semina hiyo iliyohudhuriwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, mawaziri, makatibu wakuu na viongozi wengine waandamizi wa serikali, Issa alieleza uzoefu wa mwaka mmoja wa utekelezaji wa BRN Tanzania Bara. Alisema mafanikio mengine mbali na nidhamu ya utendaji na mfumo uliowekwa ya BRN kwa Tanzania Bara, yametokana pia na vipaumbele vichache vinavyogusa sekta muhimu kwa taifa.
Alitaja baadhi ya mafanikio ambayo yamepatikana kupitia mfumo huo wa BRN kwa Tanzania Bara kuwa ni sekta ya maji, uchukuzi na nishati. Katika semina hiyo, mtaalam ambaye pia ni Waziri Katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na Mkuu wa Kitengo cha Utekelezaji wa Miradi ya Kipaumbele nchini humo (Pemandu), Dk. Idris Jalla, alisema serikali nyingi duniani zina mipango mingi mizuri, lakini utekelezaji wake umekuwa ni tatizo.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment