Social Icons

Pages

Monday, January 05, 2015

MAHAKAMA KUAMUA LEO KESI YA KINA MDEE

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam inatarajiwa leo inatarajiwa kuamua kama Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na wenzake wanane wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wanaokabiliwa na mashitaka ya kutotii amri halali ya Jeshi la Polisi na kufanya mkusanyiko isivyo halali kwa lengo la kwenda Ikulu wama kesi ya kijibu ama la.
Mbali na Mdee, washtakiwa wengine ni Rose Moshi (45), Renina Peter, Anna Linjewile (48), Mwanne Kassim (32), Sophia Fangel (28), Edward Julius (25), Martha Mtiko (27) na Beatu Mmari (35). Desemba 16, 2014, Mdee na wenzake walisomewa maelezo ya awali na mawakili wa Serikali Ahmed Salim na Wakili Mwandamizi Tumaini Kweka walidai mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Kaluyenda, kwamba washtakiwa hao walikamatwa katika Mtaa wa Ufipa wakiwa wamebeba mabango, lakini walikana mashtaka yote.
Mawakili hao walidai washtakiwa hao walikaidi amri halali ya Polisi iliyowataka kutawanyika baada ya wafuasi hao kutaka kutembea kwenda kumuona Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kupinga Katiba Inayopendekezwa.
Wakili Salim alidai baada ya kukaidi kufuata amri hiyo, iliwalazimu polisi kutumia nguvu kuwatawanya kwa kosa la kufanya fujo. Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala, aliiomba mahakama hiyo kuwafutia wateja wake shtaka la pili kwamba washtakiwa hao kwa pamoja walikusanyika kwa lengo la kutembea kwenye Ofisi ya Rais kwamba shtaka hilo lina mapungufu kisheria kwa kuwa hakuna vifungu vilivyoainisha kosa hilo.
Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa, Oktoba 4, mwaka jana washtakiwa wakiwa Mtaa wa Ufipa, bila kuwa na uhalali walikiuka amri halali ya kutawanyika iliyotolewa na Mrakibu wa Polisi (SP), Emmanuel Tillf, kwa niaba ya Jeshi la Polisi. Ilidaiwa kuwa washtakiwa hao walitenda  kosa hilo kinyume cha kifungu cha 124 cha Sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Katika shtaka la pili, washtakiwa hao wakiwa eneo hilo, walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo moja la kutembea kwenda Ofisi ya Rais, huku wakijua ni kinyume cha sheria.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments: