Pages

Saturday, January 03, 2015

JK ATEUA MWENTEKITI MPYA BODI YA TANESCO



Rais Jakaya Kikwete amemteua Dk Mighanda Manyahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Mstaafu Robert Mboma aliyemaliza muda wake.
Baada ya uteuzi huo, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amewateua wajumbe wanane watakaounda Bodi hiyo ambao ni Kissa Kilindu, Juma Mkobya, Dk Haji Semboja, Shaaban Kayungilo, Dk Mutesigwa Maingu, Boniface Muhegi, Felix Kibodya na Nyamajeje Weggoro.
Akithibitisha uteuzi huo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava alimwambia mwandishi wa gazeti hili kuwa uteuzi huo umefanyika na tayari wajumbe wameshaanza kazi kama walivyopangiwa.

CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment