Baada ya miaka kadhaa ya matokeo yasiyo na matumaini, Timu ya Taifa ya
Afrika Kusini Bafanabafana inakwenda katika fainali za michuano ya
kuwania kombe la Afrika la mataifa kwa kujiamini.
Wakati ikiweka matumaini hayo bado inakumbuka msimu mbaya uliomalizika
mwaka 2014 kutokana na kifo cha nahodha na mlinda mlango wa timu hiyo
Senzo Meyiwa, ambae aliuwawa katika tukio la ujambazi mwezi Oktoba.Hivi sasa ikiwa ni sura tofauti kwa mabingwa wa wa Kombe la mataifa ya
Afrika1996 chini ya kocha mpya Anatikisa Mashaba. Bfana Bafana
hawajapoteza nafasi katika michezo 11 na wanajiamini kabla ya mashindano
yatakayoanza huko Guinea ya Ikweta Jumamosi ijayo Januari 17.
‘Mwaka wa 1996 tulionesha kiwango kuwa sisi ni timu ya kuwa bingwa na ya
ushindani'Mashaba aliwaambia waandishi wa habari mjini Johannesburg
kabla ya timu kuondoka kwenda mashindanoni.
Kwenye timu tunajaribu kufufa moyo wa ushindani na kuonesha kuwa ni moja kati ya zile timu bora.
Bafana Bafana (Vijana, Vijana) kama ambavyo timu hiyo
inajulikana, itaanza mashindano kwenye kundi C kwa mchezo wake dhidi ya
Algeria timu iliorodheshwa kuwa namba moja Afrika- pambano
litakalofanyika kwenye mji wa Mongomo siku ya Jumatatu, Januari 19.
Mechi nyingine za kundi hilo ni dhidi ya Senegal tarehe 23 Januari na
Ghana tarehe 27 Januari kwenye kile kinachoonekana kama kundi la kifo.
David Minchela, mwandishi wa habari kutoka gazeti la michezo linalongoza
Afrika Kusini -Laduma, anaamini kuwa matamshi ya kujiaamini kupindukia
kutoka kwa kocha Mashaba yametowa mtihani kubwa kwa wachezaji. ‘Hatujawahi kuwa na timu bora na ngumu kwa hiyo kuweka matarajio makubwa
ya namna hiyo kwenye timu, naamini Kocha ataifanya Bafana ianguke'
alisema Minchela.
"Tutaondolewa mashindanoni kwenye raundi ya kwanza – Samahani kwa kusema
hili,Urahisi wa kufaulu ni kama ndoto za alfajiri" Afrika Kusini
haijawahi kukabiliana na shinikizo tokea walipoanza kushinda mchezo wao
wa kwanza, aliongeza Minchella."Tukikutana na upinzani, huwa
tunaporomoka“.
Bafana wameshindwa kufanya vizuri tokea waliposhinda AFCON
1996, licha ya kuwa moja kati ya timu inayopewa rasili mali za kutosha
Afrika. Kwa sasa wako nafasi ya 51 kwenye orodha ya timu bora duniani.
Mauaji ya nahodha na kipa Senzo Meyiwa na majambazi mwishoni mwaka jana
jijini Johannesburg na ushauri wa nguvu kutoka kwa Mashaba kunaonekana
kuiimarisha timu.
Kipa Meyiwa alipigwa risasi mbele ya mpenzi wake wakati wawili hao
wakiingia kwenye nyumba moja katika kitongoji cha jiji hilo la
Johannesburg karibu saa 2 usiku Oktoba 26.
Kocha Mashaba mwenye umri wa miaka 63, aliyechukua nafasi ya Gordon
Igesund Julai mwaka jana, amewahi kuifundisha Bafana kati ya 2002 hadi
2004. Maandalizi kwa ajili ya mashindano ya Bafana yalianza Januari na ushindi
wa 1-0 dhidi ya mabingwa wa zamani wa Afrika Zambia katika mechi
iliyochzwa Johannesburg.
Jumapili iliopita , walitoka sare 1-1 na Cameroon kwenye mechi nyingine ya kujipima nguvu. Wachezaji wengi wakiwamo mshambulizi Bernard Parker, viungo Thuso Phala, Sibusiso Vilakazi and Bongani Zungu wameonesha viwango vya juu wakati Mashaba akijaribu mbinu tofauti.
Jumapili iliopita , walitoka sare 1-1 na Cameroon kwenye mechi nyingine ya kujipima nguvu. Wachezaji wengi wakiwamo mshambulizi Bernard Parker, viungo Thuso Phala, Sibusiso Vilakazi and Bongani Zungu wameonesha viwango vya juu wakati Mashaba akijaribu mbinu tofauti.
CHANZO: DW KISWAHILI
No comments:
Post a Comment