
Wakazi wa Feri, Dar es Salaam, wameiomba Serikali
kukifanyia marekebisho kivuko cha MV Magogoni kinachofanya safari zake
kati ya Kivukoni na Kigamboni ambacho kimekuwa kilaharibika kila mara
na kusababisha usumbufu kwa abiria.
Hatua hiyo imefuatia matukio ya kuharibika mara kwa mara nyakati za
usiku na kuchukua muda majini huku kikiwa na abiria na magari.
Fadhili Mbaga, mkazi wa Kigamboni, alisema, Serikali inapaswa
kuangalia kwa makini suala la usalama wa abiria wa Feri ambao wanatumia
usafiri huo, kutokana na kivuko hicho kutokuwa na sifa za kusafirisha
abiria wengi na mizigo kwa wakati. “Abiria tumekuwa na wasiwasi na huu usafiri kwani mara nyingi
injini ya kivuko hiki siyo nzima na kusababisha ofu kubwa kwetu,”
alisema.
Anna Mwasombe, mwanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere, alisema kutokana na ubovu wa kivuko hicho, abiria wengi
wasiokuwa na haraka hulazimika kusubiri kupanda kivuko cha Mv Kigamboni. “Mara nyingi kivuko hiki kikiwa kinafanya safari zake hutumia saa
nyingi kufika upande wa pili kutoka na kuelemewa, hivyo kusababisha
abiria kutumia muda mrefu kufika kutokana na kutembea taratibu,”
alisema.
Samson Gama, alisema Serikali kwa kushirikiana na Wakala wa Ufindi
na Umeme (Temesa) inapaswa kufanya ugaguzi kila wakati ili kuhakikisha
vivuko vyote vinakuwa katika hali nzuri na salama kusafirisha abiria. Hata hivyo, NIPASHE ilimtafuta Afisa Habari Temesa kutolea
ufafanuzi kuhusiana na malalamiko hayo, lakini simu yake haikupatikana.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment