Pages

Wednesday, December 24, 2014

WATEGA AIRTEL KUTUMA PESA BURE

Mkurugenzi wa Mawasiliano, Beatrice Singano.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, kwa mara nyingine tena imewazawadia wateja wake wakati wa msimu huu wa sikukuu na ofa maalum itakayowawezesha kutuma pesa bila kikomo bure kupitia huduma ya Airtel Money.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Beatrice Singano, alisema wameona vyema kuwazawadia wateja wao nchini kote na kuwawezesha kutuma pesa bure wakati wa msimu huu wa sikukuu. Singano alisema hatua inatokana na kampuni nhiyo kutambua kuwa wateja wao na Watanzania, hufanya miamala ya pesa kwa wingi wakati wa kipindi cha msimu wa Sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya na kusherehekea nao. "Kuanzia sasa, wateja wetu watatuma pesa kwa ndugu, jamaa na familia popote nchini Airtel – Airtel bure kabisa," alisisitiza.
Aliongeza: "Hii ni nafasi pekee kwa wateja wetu na tunaamini kabisa kwamba ofa hii itawapatia wateja wetu thamani ya pesa zao na kuwawezesha kupata pesa ya akiba kwa matumizi mengine katika msimu huu wa sikukuu.”
Singano alifafanua kuwa pamoja na ofa hiyo, pia ya Airtel Money  imewazawadia wateja wao katika msimu huu wa sikukuu na ofa kabambe ya simu za kisasa kwa ajili ya wapendwa wao zinazopatikana katika maduka ya kampuni hiyo. Alisema ili kufurahia ofa hiyo ya Airtel Money, mteja anatakiwa kupiga *150*60# na moja kwa moja atakuwa ameunganishwa na orodha ya huduma za Airtel Money na kutuma pesa sehemu yoyote  bure na kwamba ofa hiyo itadumu kwa mwezi mmoja.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment