Louis
van Gaal ameteuliwa kuwa kocha bora wa mwaka wa Uholanzi baada ya
kuliongoza taifa hilo kufika nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia
nchi Brazil.
Kocha huyo aliacha kazi ya kuinoa timu ya taifa baada
ya kupata dili la kuwa kocha wa klabu ya Manchester United alikabidhiwa
tuzo hiyo jana katika jiji Amsterdam nchi Uholanzi.
Winga machachari wa timu ya taifa na klabu ya Bayern Munich Arjen Robben ameibuka kuwa mwanamichezo bora wa mwaka wa Uholanzi.
Huku
mshambuliaji Robin van Persie akitwaa tuzo ya goli bora kwa goli la
kichwa alilofunga kwenye michuano ya kombe la dunia dhidi yan Hispania.
Dereva
wa kinda wa fomula1 Max Verstappen,ameibuka kidedea katika tuzo za
mwanamichezo bora chipukizi, skater Ireen amekua mwanamichezo bora wa
kike baada ya kufanya vizuri kwenye michezo ya Olimpiki.
CHANZO: BBC SWAHILI

No comments:
Post a Comment