Prof. Sospeter Muhongo.
Aidha, umoja huo umetetea uamuzi wa Rais kumweka kiporo Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliakim Maswi, ambao wanaendelea kuchunguzwa na vyombo vya uchunguzi, kabla ya kuchukuliwa hatua.
Katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za UVCCM Upanga jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Idara ya Hamasa na Chipukizi ya umoja huo, Paul Makonda, alisema wamefurahishwa na hotuba ya juzi ya Rais Kikwete iliyofafanua masuala makubwa ya kitaifa likiwamo suala la akaunti ya Escrow Tegeta.
Makonda alisema Prof. Muhongo na Maswi hawapaswi kuchukuliwa hatua kabla ya kukamilika kwa uchunguzi unaofanyika dhidi yao kwa kuwa umoja huo unaamini wkuwa wawili hao walipotoshwa na maamuzi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. “Tunampongeza mheshimiwa Rais kwa kutengua uteuzi wa Tibaijuka. Tunamuomba atuteulie waziri mwingine atayeimudu ipasavyo kwa kutatatua na kumaliza kabisa migogoro ya ardhi ambayo imeendelea kusababisha vurugu, machafuko na maafa katika maeneo mbalimbali nchini kama vile Mvomero, Maswa na Kiteto,” alisema Makonda.
“Kuhusu Muhongo, waziri si mtaalam bali anapata taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu wa wizara yake. Maswi alikataa kutoa fedha na aliandika barua tatu kwenda kwa AG (Mwamasheria Mkuu wa Serikali) akiomba ufafanuzi na ushauri, lakini mwanasheria mkuu alimwandikia barua mbili akimwambia atoe hizo fedha. “Kama ni suala la kodi, si la wizara, ni la TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania). Prof. Tibaijuka kuna ushahidi wa fedha umemtia hatiani, hatia ya Prof. Muhongo imeangaliwa wapi?” alihoji Makonda.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment