Social Icons

Pages

Tuesday, December 16, 2014

SIMU TANO 'BAB KUBWA MJINI' 2014


 
Tofauti na miaka mitano iliyopita, mwaka huu ulimwengu umeshuhudia uvumbuzi wa hali ya juu katika utengenezaji wa simu za kisasa. Jambo zuri ni kuwa matoleo karibu yote ya simu hizo yalifanikiwa kuzinduliwa hapa nchini mwezi mmoja au miezi michache tu baada ya kutengenezwa na kampuni husika.

Baadhi ya Watanzania nao wamekuwa wakizichangamkia na kujumuika na ulimwengu wa teknolojia hiyo ya hali ya juu. Zifuatazo ni miongoni mwa matoleo ya simu ambayo yamebaki gumzo ulimwenguni mpaka sasa.

Huawei Ascend Mate 7
Simu hii ilikuja na teknolojia ya king’amuzi cha alama za vidole kuongeza usalama wa taarifa za mtumiaji. Simu hii inayotumia mtandao wa 4G, imekuja ikiwa katika matoleo mawili ya laini moja na mbili. Kioo chake kilichotengenezwa kwa madini ya Sapphire kina ukubwa wa nchi 6 huku uwezo wa ndani wa kuhifadhi taarifa ukiwa ni 64GB na Ram ya 3GB. Toleo hilo huenda likawa la mwisho kuzinduliwa kwa kuwa zimesalia wiki mbili mwaka uishe na hadi sasa hakuna fununu za kampuni nyingine kuzindua simu yake mpya hapa nchini.  

LG G3
Baada ya kutamba sokoni na G2, kampuni ya LG ilitoa toleo la G3 ambalo ndilo liliobaki kinara ndani kampuni hiyo hadi sasa. Watanzania wanaokwenda na wakati walianza kuzipata simu hizo sokoni kuanzia mwezi Septemba mwaka huu. G3 huenda ndiyo mshindani mkuu wa S5 kwa mwaka huu na ina kioo chenye ukubwa wa nchi 5.9. Pamoja na sifa hizo simu imeokosolewa kwa kuwa na sauti dhaifu na nyembamba ambayo baadhi wameonekana kutovutiwa nayo. Utendaji wa betri unaoenekana kuwa wa kawaida na huisha haraka pale kioo chake QHD kinapoongezwa mwanga wa juu. Hata hivyo, Meneja Mkuu wa kitengo cha simu za LG Afrika Mashariki, Hyon Kim, anaeleza kuwa wameongeza ufanisi wa betri hizo hadi uwezo wa 3000mAh ambapo chaji inadumu kwa muda mrefu.

iPhone 6 na iPhone 6 plus
Kwa mwaka huu katika nyanja za usanifu, Apple walitia fora. Hiyo ndiyo lugha rahisi unayoweza kuelezea uvumbuzi ambao kampuni imeuendeleza hata baada ya kutofanikiwa kwa kiasi kikubwa katika iPhone 5c na iPhone 5s mwaka jana. Matoleo mapya ya iPhone 6 na iPhone 6 plus yanakaribiana kwa kiwango kikubwa na kutofautiana vitu vichache, ila iPhone 6 plus ni bora zaidi kwa ukubwa wa kioo cha nchi 5.5 dhidi ya 4.7. Hata hivyo, siku kadhaa baada ya kuanza kuuzwa zilizuka taarifa za iPhone 6 plus kujipinda ikiweka kidogo mfukoni na kukaa kiasi cha kuwashtua wengi waliokuwa wamezinunua au waliokuwa na mpango wa kuzinunua. Wataalamu mbalimbali walionyesha kupitia vyombo vya habari vya kimataifa namna simu hiyo ilivyokuwa ikijikunja kidogo kutokana na  wa kasha lake la bati kuwa laini.

Samsung Galaxy S5
Ubunifu wa hali ya juu. Hilo neno uanaloweza kuzungumza katika uvumbuzi ulifanyika katika simu hii dada wa Galaxy S5. Ni simu ya wenye fedha na wanaotaka kurahisha kazi zao kupitia viganja. Simu hii iliongezwa ulinzi kwa kuwekewa king’amuzi cha ulinzi na programu lukuki za kiafya na kikazi. kiwango kikubwa na kutofautiana vitu vichache, ila iPhone 6 plus ni bora zaidi kwa ukubwa wa kioo cha nchi 5.5 dhidi ya 4.7. Hata hivyo, siku kadhaa baada ya kuanza kuuzwa zilizuka taarifa za iPhone 6 plus kujipinda ikiweka kidogo mfukoni na kukaa kiasi cha kuwashtua wengi waliokuwa wamezinunua au waliokuwa na mpango wa kuzinunua. Wataalamu mbalimbali walionyesha kupitia vyombo vya habari vya kimataifa namna simu hiyo ilivyokuwa ikijikunja kidogo kutokana na  wa kasha lake la bati kuwa laini. Katika mitandao mbalimbali ya kutathmini simu kama TechRadar, S5 imepata nyota 4.5 hususan katika suala la utendaji, matumizi na thamani yake. Moja ya sifa kuu iliyoibeba simu hii ni kasi ya kuchakata taarifa, ukubwa na uangavu wa kioo, betri na programu rafiki kwa matumizi ya kila siku. Tovuti maarufu ya kupitia vifaa vya simu ya technobezz lilibaini kuwa pamoja na ubora wa Samsung wengi hawakutarajia kama ingeendelea kutoa makasha ya plastiki na pia usomaji wake wa alama za vidole kwamba ungesumbua kutokana programu inayoendesha kuwa dhaifu.

Sony Experia E3
Sony haikutaka mwaka upite bila matoleo kadhaa na Septemba ilizundua simu aina ya Experia E3 ambayo ndiyo kinara wake kwa sasa. E3 yenye kioo cha nchi 4.5 na kamera yenye megapixel 5 imeongezwa ubora na inajumuisha asilimia kubwa ya huduma zilizokuwa kwenye mfululizo wa Z. Sony imeiita simu hiyo kuwa toleo la vijana kutokana na usanifu wake ulioifanya ionekane vizuri. Hata hivyo, E3 ubora wa betri upo chini kidogo ukifananisha na Samsung Galaxy 5.

CHANZO: MWANANCHI

No comments: