Rais Kikwete akipata somo kutoka kwa mwanafunzi
Mfuko wa Rais wa Kujitegemea
(PTF) utatoa mikopo kwa wahitimu wa vyuo vinavyotambuliwa na Mamlaka ya
Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Tanzania (Veta) kuanzia Januari mwakani.
Ofisa Uendeshaji na Masoko wa PTF, David Maluila
alisema katika semina ya wanufaikaji wa mkopo huo wenye masharti nafuu
kuwa wahitimu watatakiwa kuunda vikundi vya watu watano na kiingilio ni
Sh5,000.
Alisema riba kwa kila mkopo ni asilimia mbili huku kiwango cha mwisho cha kukopa ni Sh500,000.
“Mikopo hii itawahusu wale tu wenye biashara, kama
tukimpa urejeshaji wake ukiwa mzuri, basi tunampa zaidi ya hapo. Lakini
tunaandaa mafunzo ya siku saba yatakayowawezesha kutambua umuhimu wa
kuchukua mkopo,” alisema Maluila.
Alisema mikopo hiyo itatolewa nchi nzima isipokuwa itaanzia Kanda ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Makambako. Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam, Ramadhan
Dongwala alisema kutokana na mkopo huo kuwalenga wahitimu wenye
biashara, utaratibu unaandaliwa ili wasiokuwa na biashara pia wanufaike.
Mshiriki wa semina hiyo, Juma Omary alisema:
“Mikopo hii ni mizuri, itatuinua kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Kama ulivyosikia riba itakuwa chini.
“Ni jambo jema, lakini utaratibu wa kila mmoja kunufaika uandaliwe usiishie tu kwa hawa wenye biashara.”
Frank Mwaisemba alisema: “Nimekuwa nikikopa benki,
lakini huu ni mkopo wa gharama nafuu kuanzia riba na ada zake,
ninawasihi wenzangu wajitokeze kuchukua mikopo hii.”
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment