Mabingwa watetezi Real Madrid watakuana na Schalke 04, Barcelona
watashuka dimbani na Manchester City na Chelsea watamenyana na Paris
Saint Germain katika mechi tatu ambazo ni marudio ya msimu uliopita.
Real Madrid iliibumburusha Schalke kutoka duru ya 16 za mwisho kwa
kuwafunga jumla magoli 9 - 2, wakati Barcelona wakipata ushindi wa 4 - 1 dhidi ya Manchester City nao Chelsea wakawapiga PSG kwa sheria ya magoli
ya ugenini katika robo fainali.
Borussia Dortmund iliibwaga Juventus magoli matatu kwa moja katika
fainali ya mwaka wa 1997, na timu hizo mbili zimepangwa kupambana tena.
Makamu bingwa wa msimu uliopita Atletico Madrid watakutana na Bayer
Leverkzsen katika mchuano mwingine kati ya Uhispania na Ujerumani.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger atamenyana na klabu yake ya zamani AS
Monaco, katikamchuano wa ushindani kwa mara ya kwanta wakati washindi
mara tano Bayern Munich wakipangwa kupambana na Shakhtar Donetsk. Klabu
ya Uswisi Basel ikashuka dimbani na Porto ya Ureno.
Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa Februari 17/18 na Feb 24/28 wakati
za mkondo wa pili zikichezwa mnamo Machi 10/11 na Machi 17/18 mwaka
ujao. Fainali itakuwa mjini Berlin Juni 6.
Na katika dimba la Europa League, bingwa mtetezi Sevilla atachuana na
Borussia Moenchengladbach katika hatua ya 32 za mwisho. Celtic imepangwa
kupambana na Inter Milan. Pia mabingwa mara tano wa Ulaya Liverpool
watachuana na Besiktas, Tottenham itachuana na Fiorentina na Napoli
itacheza na Trabzonspor.
Katika mechi nyingine, Roma itakuana na Feyenoord, Ajayx dhidi ya Legia
Warsaw na Everton itampambana na Young boys. Huku UEFA ikizitenganisha
timu za Urusi na Ukraine kwa sababu za kisiasa, Zenit St Petersburg
imepangwa na PSV Eindhoven. Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa
Februari 19 na ya marudio zikichezwa Februari 28.
CHANZO: DW KISWAHILI

No comments:
Post a Comment