
Hata hivyo, Maranda alishindwa kuhudhuria mahakamani hapo kutokana na matatizo ya kiafya huku wenzake wanne walifikishwa kizimbani ambao ni Farijala Hussein, Iman Mwakosya, Ester Kanoni na Bosco Kimera.
Hakimu Mkazi, Ignas Kitusi, akisaidiana Eva Nkya, aliueleza upande wa utetezi kuwa ushahidi uliowasilishwa unakinzana na maelezo ya barua iliyoandikwa na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dk. Marina Njelekela kueleza kuwa Maranda hakulazwa hospitalini hapo.
Kitusi aliutaka upande wa utetezi kuwasilisha barua ya Moi itakayoeleza ni kwa muda gani alikaa hospitalini na kama kuna haja ya kwenda kutibiwa nje ya nchi ili Mahakama ijue utaratibu wa kuiendesha kesi hiyo.
Desemba Mosi mwaka huu, Maranda alitakiwa kufika mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa kesi hiyo, lakini alishindwa kufika kwa madai ya matatizo ya kiafya na kuilazimu Mahakama kuipangia jana.
Upande wa utetetezi wa serikali uliwakilishwa na wakili Fredrick Kimaro huku upande wa mashtaka akiwamo wakili Kung’e Wabeya.
Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka ya kuwasilisha nyaraka za uongo, kughushi, na kuiba jumla ya Sh. Milioni 207.
Washtakiwa wanadaiwa kughushi nyaraka ambazo ni pamoja na hati za makubaliano ya kuhamishwa deni kutoka kampuni ya General Marketing ya India kwenda Kampuni ya Rashaz (T) ya Tanzania, ambazo walizitumia na kuiba fedha hizo.Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Desemba 19, mwaka huu.
CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment