Maafisa
wakuu wa shirikisho la FIFA wamekubaliana kuchapisha ripoti yote kuhusu
uchunguzi wa madai ya ufisadi uliotokea wakati wa kutolewa kwa
kandarasi za kombe la dunia kwa mataifa ya Urusi mwaka 2018 na Qatar
mwaka 2022.
Wamekubaliana kutoa kurasa 430 za uchunguzi wa Michael
Garcia baada ya kufanya mkutano kufuatia pendekezo la mkuu wa kufuata
maagizo Domenica Scala. Ripoti hiyo itawekwa wazi baada ya
uchunguzi unaondelea kuhusu watu watano kukamilika na inatarajiwa
kufanyiwa uhariri ili kuficha majina ya mashahidi. Hatua hiyo ya
kuichapisha ripoti hiyo inaonyesha mabadiliko ya sera baada ya FIFA
kukataa shinikizo kutoka kwa Garcia mwenyewe na wengine kutoa ripoti
hiyo. Garcia alijiuzulu siku ya Jumatano baada ya ombi lake la
kupinga ripoti fupi ya uchunguzi wake iliotolewa na mwenyekiti wa kamati
ya maadili katika shirikisho hilo Hans-Joachim Eckert kukataliwa.
CHANZO: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment