Habari kutoka kijijini humo zilizothibitishwa na Katibu wa CUF wilayani
humo, Said Katundu, zilieleza kuwa mgombea wa chama hicho, Fadhili
Ngumbila, ameshinda nafasi ya Mwenyekiti kwa kujizolea kura 217 dhidi ya
mgombea wa CCM, Hamikdu Bea, aliyepata kura 160.
Katundu alisema licha ya uchaguzi huo, pia zilishindaniwa nafasi nne za wenyeviti wa vitongoji. Vyama vya CCM, CUF, NCCR-Mageuzi na Chadema, vilisimamishja mgombea wake ambapo kila kimoja kimefanikiwa kupata kitongoji kimoja. Alivitaja vijiji ambavyo vimeshinda katika nafasi ya uenyekiti kuwa Mungurumo, Kiliowike, Makonjiganga, Mikunya, Kitamamui, Barikiwa, Kibutuka na Mirui.
Katibu huyo wa CUF wilaya alisema chama chake kimepata ushindi mkubwa kwa kujizolea vitongoji tisa kati ya 12 vilivyokuwa vikishindaniwa katika uchaguzi huo wa marudio kwenye Wilaya yote ya Liwale. Aidha, alisema kutokana na ushindi huo, CUF wilayani humo kimepanda kutoka vijiji 17 ilivyovipata mwaka 2009 hadi 37, hivyo kuongeza vijiji 20 kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Pia Katundu alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, CUF kimefanikiwa kujizoelea vitongoji 153 kati ya 351 vilivyopo wilayani Liwale.
Wilaya ya Liwale ina jumla ya vijiji 76 ambapo kati ya hivyo, CUF ilisimamisha wagombea katika vijiji 74 na kushinda 37.

CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment